Ijumaa, Mei 24, 2013 Local time: 23:34

Habari / Afrika

Wachimbaji madini 60 wafariki DRC

Mfano wa mgodi ulioporomoka na kuwafukia wachimbaji wadogo wadogo wa madiniMfano wa mgodi ulioporomoka na kuwafukia wachimbaji wadogo wadogo wa madini
x
Mfano wa mgodi ulioporomoka na kuwafukia wachimbaji wadogo wadogo wa madini
Mfano wa mgodi ulioporomoka na kuwafukia wachimbaji wadogo wadogo wa madini
ukubwa wa habari - +
Maafisa wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC wanasema ajali ya migodi katika eneo moja dogo huko kaskazini mashariki mwa nchi hiyo imewauwa wachimba madini 60.

Maafisa wa serikali wanasema watu hao walikuwa wakichimba dhahabu kiasi cha mita 100 chini ya ardhi Jumatatu wakati mgodi ulipoporomoka na kuwafukia.
 
Eneo hilo linapakana  na  Pangoyi katika jimbo la Orientale. Maafisa  wanasema eneo hilo linadhibitiwa na wanamgambo na kwamba wametatiza  juhudi za waokozi.

Maelfu ya watu katika nchi hiyo maskini wanajaribu kutafuta riziki zao za kila siku kwa kufanya kazi katika maeneo yasiyo salama ambayo yanahusisha uchimbaji mdogo mdogo wa madini. Ajali za mara kwa mara nchini humo katika eneo la migodi ni jambo la kawaida.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--