Alhamisi, Februari 11, 2016 Local time: 00:57

  Habari / Afrika

  Wabunge wanawake wa Somalia wakutana

  Wanawake wa Somalia mjini Mogadishu
  Wanawake wa Somalia mjini Mogadishu
  Kuna usemi kuwa “Ukimuelimisha mwanamke umeelimisha  jamii nzima”. Hii ndio sababu wabunge wanawake  kutoka Somalia wanakutana mjini Kampala kujadili shida zinazowakumba. Lengo lao likiwa  kuhakikisha wanawake wanajumwishwa kikamilifu kwenye maamuzi na utungaji wa sheria za Somalia kwa sababu kina mama wanazielewa  shida zinazoikumba jamii na njia bora za kuzitatua .

  Leyla Ndinda, kampala-Uganda
  Leyla Ndinda, kampala-Ugandai
  || 0:00:00
  ...    
   
  X

  Somalia iliunda serikali mpya mwezi wa nane mwaka 2012 miaka 21 baada ya kukosa uongozi mwafaka wa kisiasa kufuatia kung'olewa mamlakani rais Siad Barre mwaka wa 1991.Wanajeshi mbali mbali kutoka mashariki mwa Afrika chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika Amisom kuanzia mwaka wa 2007 walikwenda Somalia kuisaidia serikali ya mpito  kudumisha amani.

  AMISOM iliweza kuyakomboa maeneo kadhaa ya Somalia kutoka mikononi mwa waasi wa Al-shabaab na hatimaye mwezi wa nane  Agosti 2012, Somalia ikaunda serikali na bunge mpya. Bunge lililoundwa lina wabunge 275.

  Ingawa wanawake waling'ang'ana ili angalau wapate asilimia thelatini ya uwakilishi bungeni, hilo halikufanyika. Walipata asili mia kumi na nne peke yake. Asili mia kumi na nne ikiwa ni wanawake 38. Ishirini na nane kati ya wanawake hawa sasa wako mjini Kampala kuhudhuria mkutano wa siku tatu wa wabunge wa kike wa Somalia.

  Wabunge wengine wa kike wanaoshiriki  wanatoka Burundi, Djibouti, Kenya, Rwanda na Uganda. Nchi hizi zote isipokuwa Rwanda zina majeshi yake nchini Somalia kuisaidia serikali ya Somalia  kudumisha amani.

  Lydia Wanyotu kutoka Uganda ambaye kwa wakati mmoja alikuwa mbunge wa bunge la Afrika mashariki anasema  mkutano huu uliandaliwa na kitengo cha jinsia cha AMISOM. Naye  naibu mkuu wa AMISOM Wafula Wamunyinyi  anasema mojawapo ya  juhudi zao ni kutekeleza jukumu walilopewa na baraza la Usalama la Umoja wa Afrika na kuidhinishwa na Umoja wa Mataifa.

  Hapo mwanzoni jukumu la AMISOM lilikuwa kuwalinda viongozi na taasisi za serikali pamoja na kusaidia kwenye mchakato wa mazungumzo na kuridhiana wakati wa serikali ya mpito. Pia walipewa jukumu la kutoa msaada wa kibinadamu na kuzijenga taasisi za serikali haswa zile za usalama na  kuboresha utendaji kazi kwenye ofisi za serikali.

  Mkutano huu ni mojawapo wa majukumu ya AMISOM kuhakikisha kuwa serikali mpya ambayo itaongoza Somalia kwa kipindi cha miaka minne ijayo inaleta amani ya kudumu na kujenga mazingira mazuri ambayo yatawawezesha wasomali wanaoishi ugenini kurudi  Somalia  ili kuijenga nchi yao.

  You May Like

  Jioni

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
  VOA Express

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
  Alfajiri

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

  mjadala huu umefungwa
  Maoni
       
  Hakuna mtu ameandika maoni hapa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.