Alhamisi, Mei 23, 2013 Local time: 18:32

Habari / Afrika

Waasi wajongea karibu na mji mkuu Bangui

Waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wasema wataingia mji mkuu Bangui licha ya kukubali kufanya mazungumzo na serikali Januari.

Rais Francois Bozize akizungumza na wafuasi wake, Desemba 27, 2012.Rais Francois Bozize akizungumza na wafuasi wake, Desemba 27, 2012.
x
Rais Francois Bozize akizungumza na wafuasi wake, Desemba 27, 2012.
Rais Francois Bozize akizungumza na wafuasi wake, Desemba 27, 2012.
ukubwa wa habari - +
Waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wanaonya kuwa wataingia katika mji mkuu Bangui hivi karibuni, licha ya makubaliano kati yao na serikali kuwa watafanya mazungumzo  yasio ya masharti mapema  Januari. Jumapili mitaa ya mji mkuu haikuwa na watu na wakazi wengi mjini humo walisema wamenunua vyakula na bidhaa za kimsingi na kuvihifadhi  wakihofia kuwa waasi  huenda wakaingia mjini humo. Tishio la waasi hao limetolewa wiki tatu baada ya kuanza maasi  dhidi ya serikali. Katika kipindi hicho wamedhibiti thuluthi moja ya nchi na kuwalazimisha wanajeshi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati kurudi nyuma hadi mji wa Damara, mji unaopakana na mji mkuu Bangui yapata kilomita  75 tu. Mkuu wa Umoja wa Afrika kwa sasa Thomas Yayi Boni anatazamiwa kwenda nchini humo  kukutana na rais Francois Bozize, katika juhudi za kuanza upya mazungumzo ya amani na Seleka, kundi mseto la waasi wenye silaha nchini humo. Seleka linashtumu rais Bozize kwa kushindwa kutekeleza kikamilifu mkataba wa amani  uliofikiwa mwaka wa 2007. Mkataba huo ulijumwisha makubaliano ya kuyashirikisha makundi ya wapiganaji kwenye jeshi la kitaifa na kuwalipa ikiwa watakaosalimisha  silaha zao  kufuatia  maasi  ya  hapo awali.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--