Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 16:28

Viongozi wa MRC wataka mahakama iwapunguzie dhamana


Omar Mwamnuadzi (kati), kiongozi wa kundi linalotaka Pwani kujitenga la Mombasa Republican Council (MRC) akiwasili katika kizuizi cha mahakama Mombasa pamoja na wenzake. October 15, 2012.
Omar Mwamnuadzi (kati), kiongozi wa kundi linalotaka Pwani kujitenga la Mombasa Republican Council (MRC) akiwasili katika kizuizi cha mahakama Mombasa pamoja na wenzake. October 15, 2012.
Wanachama wa kundi la vuguvuvugu nchini Kenya lijulikanalo, Mombasa Republican Council –MRC waliokamatwa mwezi uliopita na kushtakiwa na serikali ya Kenya kwa madai ya uchochezi, wengi wameshindwa kupewa dhamana na huenda wakasalia gerezani kwa muda mrefu.

Mashtaka dhidi ya wanachama wa MRC yameibua hisia tofauti miongoni mwa wa-kenya. Kwanza ni usalama wa kitaifa, japo hatua ya kuwanasa viongozi wakuu wa kundi hilo inaonekana kama ni njia moja ya kusambaratisha kundi hilo.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:53 0:00
Kiungo cha moja kwa moja



Kabla ya serikali kuwanasa wanachama wa MRC mwezi uliopita, kundi hilo lilikuwa limesajili wanachama wengi katika kila wilaya ya mkoa wa Pwani, na hata kushinda awamu ya kwanza ya kesi dhidi ya serikali, na kuondolewa katika orodha ya makundi haramu.

Lakini majuma mawili yaliyopita serikali ilipiga marufuku msimamo wa kusema Pwani Si kenya, na yeyote aliyepatikana akieneza ujumbe huo alikamatwa na kupelekwa rumande.

Dhamana waliyopewa washtakiwa hao mahakamani ni ya juu mno, na wengi wameshindwa kulipa, huku mawakili wao wakiishia kutuma maombi kortini karibu kila siku, viongozi hao wa MRC wapunguziwe dhamana – kati ya shilingi millioni 1 na millioni mbili za Kenya.

Hapo jana zaidi ya watu 20 wamejitokeza kwa maafisa wa usalama pamoja na wabunge wa pwani, wakisema wao ni waanchama wa MRC, lakini wanakubali kushirikiana na serikali kudumisha usalama.

Badala ya Pwani Si Kenya, walivalia fulana zenye maandishi PWANI NI KENYA, katika mkutano wa amani uliokuwa ukifanyika katika jimbo la Kilifi, ambako walipokelewa na waziri wa usalama wa ndani Ole Metito.

Mbunge mmoja Mike Mbuvi amejitolea kuwalipia dhamana viongozi wakuu wa MRC walioshindwa kutoka kizuizini kwa sababu ya udhamini. Bwana Mbuvi amechukua hatua hiyo na anataka viongozi hao wakubali kufanya mazungumzo na serikali kwa kulegeza masharti ya vuguvuvu hilo.

Viongozi walioshtakiwa ni mwenyekiti Omar Mwamnuadzi na mke wake, katibu Randu Nzai na msemaji wa MRC, Rashid Mraja.
XS
SM
MD
LG