Alhamisi, Aprili 02, 2015 Local time: 12:42

Habari / Afrika

Viongozi wa Ansar Dine wakamatwa Mali

Wapiganaji wa kundi la Ansar Dine wakiwa TimbuktuWapiganaji wa kundi la Ansar Dine wakiwa Timbuktu
x
Wapiganaji wa kundi la Ansar Dine wakiwa Timbuktu
Wapiganaji wa kundi la Ansar Dine wakiwa Timbuktu
Maafisa wawili waandamizi wa wanamgambo wa kislamu wamekamatwa huko kaskazini mwa Mali akiwemo kiongozi mmoja wa cheo cha juu wa kundi la ki-Islam lenye msimamo mkali la Ansar Dine.

Maafisa wa kundi la Wa Tuareg wanaotaka kujitenga kutoka Mali cha  MNLA linasema liliwakamata Mohamed Moussa Ag Mohamed na Oumeini Ould Baba Akhmed siku ya jumamosi karibu na mpaka wa Mali na Algeria.

Ag Mohamed ni kiongozi wa tatu wa kundi la Ansar Dine na alisaidia katika utekelezaji wa sheria kali ya Ki-islam katika mji wa Timbuktu.

Baba Akhmed inaaminika kuwa mwanachama wa kundi la Movement for Unification and Jihad katika Afrika Mashariki lijulikanalo pia kama MUJAO.

Makundi hayo mawili pamoja na al-Qaida katika nchi za Afrika  Maghreb walidhibiti miji mikubwa ya kaskazini mwa Mali kwa kiasi cha miezi tisa kabla ya kuondolewa na wanajeshi wa Ufaransa na Mali.
 
Ndege za kivita za Ufaransa ziliendelea kufanya mashambulia ya mabomu dhidi ya makundi ya ki-Islam siku ya Jumapili wakishambulia njia za kusafirisha vifaa na vituo vya kutoa mafunzo katika eneo la mbali katika jangwa la kaskazini-mashariki mwa Mali. Waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa, Laurent Fabius alisema lengo ni kuharibu kambi na ghala za wanamgambo, hivyo washindwe kuendelea kuwepo tena huko kaskazini mwa Mali.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Uvutaji sigara hadharani wakemewa Tanzaniai
|| 0:00:00
...  
🔇
X
01.04.2015 14:12
Ingawa serikali ya Tanzania haijaweka sheria dhidi ya uvutaji sigara hadharani watu wengi wanakemea tabia hiyo kuwa ina madhara hata kwa wasiovuta.