Jumatatu, Mei 25, 2015 Local time: 02:08

Habari / Afrika

Viongozi wa Afrika watoa wito kwa wapiganaji wa M23 kuondoka Goma

Wacongo wakimbia vita kutoka mji wa Sake, 27km magharibi ya Goma, Nov. 23 2012.
Wacongo wakimbia vita kutoka mji wa Sake, 27km magharibi ya Goma, Nov. 23 2012.
Viongozi wa mataifa ya Afrika Mashariki na Kati walikutana Jumamosi mjini Kampala  kujaribu kutanzua mzozo unaoendelea mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mkutano huo ulohudhuriwa na Marais wa Uganda, Tanzania Kenya na Congo ulipendekeza mpango wenye nukta nane, juu ya jinsi ya kutanzua mzozo huo.

Rais Paul Kagame ambae anatuhumiwa na ripoti ya Umoja wa Mataifa kwamba anawafadhili wapiganaji wa M23 hakuhudhuria mkutano na  katika dakika za mwisho alimtuma waziri wake wa mambo ya nchi za nje, Bibi.  Louise Mushikiwabo.

Viongozi hao wamewataka pia waasi wa kundi la M23 kusitisha mara moja mashambulizi yao na kuondoka Goma. Wamependekeza pia kuwepo na kikosi cha kimataifa kwenye uwanja wa ndege wa Goma ikiwahusisha majeshi ya Tanzania na DRC

Umoja wa mataifa imeituhumu Rwanda kwa kuwasaidia waasi hao wa M23, jambo Kigali inakanusha. Mkutano huo wa viongozi mjini kampala umefanyika kukiwa na wasi wasi kwamba waasi wanasonga mbele huko mashariki ya nchi na kukiwepo na mabadiliko katika jeshi la Congo.

Kwa upande mwengine mashirika ya misaada ya dharura yanaeleza wasi wasi wao kutokana na ukatili unaotendewa raia ambao wengi wako njiani wakikim bia vita. Kuna ripoti za maiti kuonekana njiani kati ya Goma kuelekea upande wa kusini.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.