Jumatano, Februari 10, 2016 Local time: 03:31

  Habari / Afrika

  Balozi wa Marekani Libya auawa katika shambulizi

  • Chris Stevens mjumbe wa Marekani akiwa katika hoteli ya Tibesty, Bengazi ambako ujumbe wa Umoja wa Afrika ulikuwa unakutana na viongozi wa upinzani wa Libya. (April 2011 file photo)
  • John Christopher Stevens, balozi mpya wa Marekani nchini  Libya, akisalimiana na mwenyekiti wa Baraza la Mpito la Kitaifa Libya (NTC) Mustafa Abdel Jalil (Kulia) baada ya kumkabidhi stakbadhi zake za uteuzi mjini Tripoli, June 7, 2012.
  • U.S. envoy Chris Stevens akizungumza na waandishi habari wa Libya katika hoteli ya Tibesty  (April 2011 file photo)
  • U.S. envoy Chris Stevens, katikati, akifuatana na mjumbe wa Uingereza Christopher Prentice, kushoto, akizungumza na diwani wa Misrata Dr. Suleiman Fortia, kulia, katika hoteli ya Tibesty Benghazi.
  • Wajumbe wa Uingereza na Marekani kwa wapinzani wa Libya Christopher Prentice (kushoto) na Chris Stevens wakihudhuria mkutano wa waandishi habari na kiongozi wa waasi Mustafa Abdul Jalil (hayumo kwenye picha) baada ya kukutana na baadhi ya viongozi wa nchi za Afrika  katika ngome ya waasi Benghazi
  • US diplomatic envoy to rebel held Libya Chris Stevens (R), Britain's diplomatic representative Christopher Prentice (L) and deputy chairman of the TNC Abdul Hafiz Ghoqa (C) hold candles during a memorial service for slain photojournalists Tim Hetherington
  • Jengo la ubalozi mdogo wa Marekani mjini Benghazi mashariki ya Libya likiwaka moto
  • Ubalozi mdogo wa Marekani Benghazi Libya umeharibiwa na watu walokuwa na hasira.
  • Jengo la ubalozi wa Marekani Benghazi, Libya baada ya kushambuliwa
   
  Maafisa wa Libya wanasema Balozi wa Marekani nchini Libya, Christopher Stevens, na wafanyakazi wengine wa ubalozi wameuawa baada ya kundi la watu kuvamia ubalozi mdogo katika mji wa Benghazi Jumanne usiku.

      Vifo hivyo vimetokea baada ya waandamanaji waliokasirishwa na sinema iliyotengenezwa Marekani ikimkashifu Mtume Muhammad kufyatulia risasi na kuchoma moto sehemu za ubalozi huo mjini Benghazi.

      Balozi J. Christopher Stevens, mwanadiplomasia wa siku nyingi na mmoja wa mabalozi wenye uzoefu mkubwa katika eneo hilo, alikuwa nchini humo chini ya miezi minne tu baada ya kuchukua wadhifa huo mjini Tripoli mwezi Mei.

       Waziri mdogo wa mambo ya ndani wa Libya Wanis al-Sharif alisema balozi huyo aliuawa "pamoja na maafisa wengine watatu," akithibitisha kuwa Stevens alikuwepo ndani ya ubalozi huo uvamizi ulipotokea.

        Sharif aliwaambia waandishi kuwa kundi la watu wenye silaha walishambulia ubalozi huo katika hali ya "kujitoa mhanga." Alisema ubalozi wa Marekani "una makosa" kwa kutochukua hatua za kutosha. Wizara ya mambo ya nje ya Marekani haijatoa tamko lolote kuhusiana na habari hiyo.

  You May Like

  Jioni

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
  VOA Express

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
  Alfajiri

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

  mjadala huu umefungwa
  Comment Sorting
  Maoni
       
  Na: DUNIA YAKUPITA Kutoka: TANZANIA
  12.09.2012 22:13
  Alhamdulillah, ALLAH awajaze kila la Kheri walibya ktk kutetea DINI TUKUFU YA UISLAM. Mlizani kuwa baada ya kumuuwa Komandoo Ghadaf basi mtatawala hadi chooni.