Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 17:45

UNICEF yasema watoto wa Sudan Kusini yawezekana waandikishwa jeshini


Picha ya maktaba ya wanajeshi wa Sudan Kusini.
Picha ya maktaba ya wanajeshi wa Sudan Kusini.

Umoja wa mataifa unaeleza kwamba hivi sasa unahofu kuwa mamia ya wavulana waliotekwa mwezi uliopita Sudan Kusini, wameandikishwa kwa nguvu kuwa wanajeshi.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, amesema shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia watoto UNICEF, linaamini idadi ya watoto waliotekwa katika jimbo la Upper Nile ni zaidi ya 89 tofati na ilivyoripotiwa.

UNICEF inaamini watoto hao waliotekwa wanatoka kundi la wanamgambo wenye uhusiano na jeshi la Sudan Kusini.

Inauhakika kundi lenye silaha linaongozwa na Johson Oloni, Jenerali ambaye alipigana dhidi ya serikali, lakini wanamgambo wake sasa wanauhusiano na jeshi la kitaifa.

Mashuhuda wanasema watu wenye silaha walizunguka kijiji cha Wu Shilluk, na kwenda nyumba kwa nyumba kutafua wavulana waliodhaniwa kuwa na miaka 12 na zaidi.

UNICEF inasema pia watu wazima walilazimishwa kujiunga na jeshi hilo.

XS
SM
MD
LG