Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:21

UKAWA wasusia kurudi bungeni Dodoma


Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma

Umoja wa katiba ya wananchi- UKAWA na Mwenyekiti wa Bunge maalum la katiba Tanzania bado wanavutana juu ya uendeshaji wa bunge hilo maalum la katiba jambo linalozusha shaka juu ya mustakbali wa upatikanaji wa katiba mpya nchini Tanzania.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:59 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Wajumbe wanaounda UKAWA chini ya uenyekiti wa mwenyekiti wa taifa wa chama cha CUF Profesa Ibrahim Lipumba wameendelea na msimamo wake wa kutokurejea katika bunge maalum la katiba linalotarajiwa kuanza tena vikao vyake Agosti tano mwaka huu, kwa siku 60 zilizoongezwa na Rais Kikwete ambapo ilitarajiwa wakikamilisha awamu hiyo itarudishwa kwa wananchi kwa ajili ya kura za maoni.

Imeelezwa kwamba ili Katiba inayopendekezwa iweze kupata uhalali wa kupitishwa kwake, sheria inaweka sharti kwamba ni lazima ikubalike na pande zote za muungano kwa zaidi ya theluthi mbili ya idadi ya wajumbe wote kwa kila upande.

Freeman Mbowe
Freeman Mbowe


Wakitoa tamko juu ya msimamo wao jijini Dar Es Salaam, Alhamis viongozi wa UKAWA akiwemo mwenyekiti wa chama cha CUF, Profesa. Ibrahim Lipumba, mwenyekiti wa chama cha CHADEMA Freeman Mbowe na mwenyekiti wa chama cha NCCR MAGEUZI James Mbatia, wamesema wako tayari kurudi bungeni pindi rasimu hiyo ya katiba iliyowasilishwa bungeni na tume ya mabadiliko ya katiba ambayo ni maoni ya wananchi, itakapojadiliwa na si vinginevyo.

UKAWA waliondoka bungeni April 16 baada ya kususia bunge maalum la katiba kwa madai kwamba bunge hilo halijadili rasimu yenye maoni ya wananchi ambayo iliwasilishwa bungeni hapo na Jaji Joseph Warioba pamoja na kulaumu kwamba bunge hilo linaendeshwa kibabe kwa kufuata matakwa ya chama tawala cha CCM kinachosisitiza kuwepo na serikali mbili ya muungano badala ya iliyopendekezwa katika rasimu ya pili ya muungano wa serikali tatu.

Hadi kikao cha kwanza cha bunge maalum la katiba huko mjini Dodoma kilipoahirishwa April 25 mwaka huu kupisha bunge la bajeti, wajumbe wa UKAWA walikuwa wamesusia vikao na kuanza kuzunguka maeneo mbalimbali nchini kuwaeleza wananchi kwamba walichosusia ni mwenendo mbovu wa bunge hilo.

XS
SM
MD
LG