Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 03:04

Uganda kuondoa wanajeshi wake Sudan Kusini


Wanajeshi wa Uganda wakiwa ndani ya kifaru katika mitaa ya Bor, Jonglei State huko Sudan Kusini
Wanajeshi wa Uganda wakiwa ndani ya kifaru katika mitaa ya Bor, Jonglei State huko Sudan Kusini

Uganda inasema inaondoa wanajeshi wake kutoka Sudan Kusini, mahala ambapo ilikuwa ikimuunga mkono Rais Salva Kiir katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Jeshi la Uganda lilisema kwamba kuondoka kwa wanajeshi wake wapatao 2,000 kutaanza Jumatatu, huku mjini kampala mkuu wa jeshi Jenerali Katumba Wamala, alisema wanajeshi hao wanatakiwa kuondoka Sudan Kusini ifikapo wiki ya kwanza ya mwezi Novemba.

Uganda ilipeleka wanajeshi wake mara tu baada ya mapigano kuzuka kati ya wafuasi wa Rais Kiir na wafuasi wa Makam Rais wa zamani Riek Machar hapo mwezi Disemba mwaka 2013. Kuondolewa kwa wanajeshi hao ilikuwa ni masharti ya mkataba wa amani uliotiwa saini na bwana Kiir na bwana Machar mwezi Agosti mwaka 2015.

Miezi 21 ya mapigano nchini Sudan Kusini iliuwa maelfu ya watu na kuwakosesha makazi kiasi cha watu milioni mbili kutoka kwenye nyumba zao. Mivutano bado ipo juu nchini humo licha ya juhudi za utekelezaji mkataba wa amani. Mapambano kati ya serikali na majeshi ya waasi yanaendelea huku kila mmoja akimshutumu mwenzake kwa kukiuka mkataba wa kusitisha mapigano.

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir.
Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir.

Wiki iliyopita Rais Kiir alitangaza Sudan Kusini itagawanywa tena katika majimbo 28 na kuwakasirisha wapinzani ambao walisema alichukua maamuzi ya upande mmoja.

Kulingana na misingi ya mkataba wa amani, pande zote zinatarajiwa kuunda serikali ya mpito hapo mwezi Novemba mwaka 2015.

XS
SM
MD
LG