Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 05:39

Theluji yatishia miji mikubwa ya Marekani


mashirika ya ndege yamesitisha kwa muda huduma zao kwa jamii
mashirika ya ndege yamesitisha kwa muda huduma zao kwa jamii

Dhoruba kubwa ya theluji inatarajiwa kuathiri sehemu kubwa ya kaskazini- mashariki mwa Marekani katika siku mbili zijazo ikianza kupiga maeneo makubwa ya mijini kutoka Washington DC hadi Boston jumatatu.

Kiwango kikubwa cha dhoruba kilikwepa mji mkuu wa Marekani lakini ilipiga upande wa kaskazini kwenye majimbo ya New Jersey, New York, Connecticut, Rhode Island na Massachusetts ambapo walitangaziwa hali ya dharura kutokana na theluji.

Mamilioni ya watu waliombwa kukaa nyumbani wakati usafiri wa reli wa Amtrack ulipunguza huduma za treni katika maeneo yenye shughuli nyingi katika ukanda wa kaskazini mashariki yaani Northeast Corridor na mashirika ya ndege yalifuta mamia ya safari za ndege katika kujiandaa na hali ya dhoruba jumatatu usiku hadi jumatano.

XS
SM
MD
LG