Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 16:33

Theluji mbaya kutokea miji ya Marekani


Miji ya New York na Boston ndio inatarajiwa kuathiriwa zaidi na theluji
Miji ya New York na Boston ndio inatarajiwa kuathiriwa zaidi na theluji

Idara ya hali ya hewa nchini Marekani imetoa onyo kwa maeneo mengi ya miji ya kaskazini-mashariki kupatwa na theluji kubwa na upepo mkali uliotarajiwa kulikumba eneo hilo jumatatu na jumanne.

Zaidi ya sentimeta 60 za theluji zinatarajiwa kunyesha katika miji na vitongoji kuanzia New York mpaka Boston na kuingia mashariki mwa Canada. Dhoruba hiyo ambayo inatokea eneo la kati nchini Marekani pia inatarajiwa kuleta theluji kusini mwa Washington DC. Lakini mji mkuu wa nchi kwa kiasi kikubwa hautakumbwa sana na theluji ambayo utabiri unaelezea itakumba zaidi maeneo ya kaskazini.

Usafiri katika maeneo ya kaskazini-mashariki kwa njia ya barabara, treni na ndege unatarajiwa kuathiriwa vibaya sana wakati dhoruba inapoelekea eneo la mashariki. Upepo mkali unavuma kwenye bahari ya Atlantik pia unaweza kusababisha mafuriko huko pwani.

Kushuka kwa theluji kunafuatia dhoruba ndogo ya awali ambayo ilisababisha sentimeta kadhaa za theluji kwenye baadhi ya maeneo ambayo yanatarajiwa kuathiriwa katika muda wa siku moja au zaidi zijazo. Maafisa wanatarajia kukatika umeme kwenye maeneo mengi kutokana na dhoruba mpya ambayo itaathiri maisha ya mamilioni ya watu.

Meya Bill de Blasio
Meya Bill de Blasio

Wakati huo huo, huko New York City, Meya Bill de Blasio aliwaambia waandishi wa habari jumapili kwamba “hii huenda ikawa moja ya dhoruba kubwa sana kati ya dhoruba mbili au tatu katika historia ya mji huu na tunahitaji kuwa na mipango kadri iwezekanavyo”. Aliwasihi wakazi wa New York kukaa mbali na barabara na “kujiandaa kwa jambo lolote baya sana ambalo hatujawahi kuliona”.

XS
SM
MD
LG