Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 14:45

Tanzania kupata msaada wa maendeleo kutoka taasisi za fedha za kimataifa


Waziri wa Fedha wa Tanzania Saada Mkuya Salum akizungumza na Mwamoyo Hamza mkuu wa Idhaa ya Kiswahili VOA
Waziri wa Fedha wa Tanzania Saada Mkuya Salum akizungumza na Mwamoyo Hamza mkuu wa Idhaa ya Kiswahili VOA
Kutokomeza umaskini barani Afrika ni mada iliyokuwa juu katika mazungumzo ya taasisi za fedha za kimataifa mjini Washington, wakati mawaziri wa fedha na wataalamu wa fedha na uchumi walipokutana kuzungumzia uchumi wa dunia.

Waziri wa Fedha wa Tanzania Saada Mkuya Salum anasema mawaziri wenzake wa mataifa ya Afrika wamejadili pamoja na wakuu wa Benki kuu ya Dunia na IMF juu ya namna ya kutumia rasilmali walonazo kutokomeza umaskini na kupunguza mwanya kati ya matajiri na maskini katika nchi zao.
please wait

No media source currently available

0:00 0:08:44 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Alipotembelea Sauti ya Amerika siku ya Jumapili baada ya kuhudhuria mikutano ya Benki Kuu ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani IMF, Bi. Salum amesema, ingawa nchi nyingi za Afrika zinashuhudia ukuwaji mzuri wa uchumi wao, mfano Tanzania ikiwa na ukuwaji wa asli mia saba ya ukuwaji, lakini mafanikio hayo hayawafiki wananchi walio wengi hasa wakulima.

Waziri wa fedha wa Tanzania anasema, nchi za kiafrika zimeshindwa kupunguza mwanya uliyopo na inabidi kuimarisha sekta ya kilimo ambao wananchi walowengi wanategemea kwa ajili ya mapato yao.

Bi Salum anasema Tanzania imepata jumla ya msaada wa dola milioni 185 kwa ajili ya miradi ya maendeleo, muhimu ikiwa msaada wa biashara kutoka IFC kuwapatia mikopo wakulima wanawake, itakayosimamiwa na benki ya CDRB Tanzania.
XS
SM
MD
LG