Jumatano, Februari 10, 2016 Local time: 21:06

  Habari / Afrika

  Somalia yapeleka balozi Afrika Kusini

   Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
  Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud
   Kwa mara ya kwanza Somalia imepeleka balozi wake Afrika Kusini, taifa lenye uchumi mkubwa barani Afrika. Balozi mpya Sayid Sheriff anasema ana matumaini makuu anapopandisha bendera ya kidiplomasia ya Somalia baada ya miongo mingi ya kutokuwa na uthabiti wa kisiasa. Anasema anapanga kuwafikia maelfu ya raia wa Somalia waliokimbilia Afrika Kusini.

  Sayid Sheriff ni balozi wa kwanza wa Somalia kupelekwa Afrika Kusini.Na kama ilivyo kawaida kwa mabalozi wanaokwenda nchini humo, alipokelewa kwa shangwe na kuandaliwa sherehe maalum. Somalia haijawa na serikali thabiti kwa miongo mingi. Ni taifa ambalo limekumbwa na ukame na njaa; vita vya wenyewe kwa wenyewe, wanamgambo wa al-Shabab wenye ushirika na mtandao wa kigaidi wa al-Qaida na tatizo la uharamia.

   Akimkaribisha balozi huyo  nchini humo  rais Jacob Zuma alisema; “Kutaabika kwao kutokana na ukame na njaa, na njia waliofikia katika kukarabati taifa lao ni njia tuliyopitia. Tutasimama nao kidete na kuwasaidia katika ujenzi mpya  wa taifa lao.”  Bwana Zuma amesema Afrika Kusini itatoa dola milioni 11 kusaidia  ujenzi mpya wa Somalia katika miundo mbinu na taasisi zake.
   
  Akizungumza na sauti ya Amerika, balozi Sheriff alisema taifa lake na Afrika Kusini zina mahusiano ya muda mrefu. Alisema zama zile Somalia ilisaidia chama cha African National Congress kupigana dhidi ya  serikali ya ubaguzi wa rangi. Lakini wakati Afrika Kusini ilipopata uthabiti wa kidemokrasia mwaka wa 1994, Somalia ilikuwa imetumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.

   Balozi  huyo  alionya kuwa mabadiliko Somalia hayatakuwa ya haraka akiashiria mlipuko wa bomu uliotekelezwa na mhanga wa kujitolea Jumanne  karibu na kasri ya rais. Alisema  baada ya vita vya zaidi ya miaka 21 vya wenyewe kwa wenyewe mabadiliko hayawezi kuonekana mara moja. Amani haitajitokeza kama muujiza, lakini Somalia inaanza kushuhudia amani hatua kwa hatua.

  You May Like

  Jioni

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
  VOA Express

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
  Alfajiri

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

  mjadala huu umefungwa
  Maoni
       
  Hakuna mtu ameandika maoni hapa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.