Jumatano, Aprili 16, 2014 Local time: 13:09

Habari / Afrika

Shule za kenya zafunguliwa rasmi 2013

Wanafunzi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, Kenya
Wanafunzi katika kambi ya wakimbizi ya Kakuma, Kenya
ukubwa wa habari - +
Shule zimefunguliwa tena nchini Kenya kwa muhula wa kwanza wa masomo mwaka huu wa 2013 lakini katika jimbo la Tana River kulikotokea ghasia za kikabila na mauaji ya watu wengi huenda wanafunzi wengi wakakosa kurejea shuleni.

Na Josephat Kioko, Mombasa
Na Josephat Kioko, Mombasai
|| 0:00:00
...
 
🔇
X

Maelfu ya watu katika sehemu hiyo ya Pwani ya Kenya wangali wanaishi kama wakimbizi wa ndani-IDP wakiwemo wanafunzi.

Awali kulikuwa na Wakimbizi wa ndani wapatao elfu 30 waliotoroka machafuko hayo, na japo idadi hiyo ilipungua bado kuna waliosalia katika Kambi hizo za muda.

Machafuko yalikumba Tana Delta tangu Agosti mwaka jana lakini wahanga walitorokea wilaya jirani za Malindi, Magarini, Kilifi, na Lamu Mashariki.
 
Kutokana na hali hiyo mwenyekiti wa muungano wa Riketa,Kilelengwani IDP Group, Abdalla Sanke huko Lamu Mashariki, anasema hofu kubwa ni kukosa nafasi za wanafunzi-wakimbizi, kuingia katika shule za karibu, na ukosefu wa ada ya shule.
 
Katika wilaya ya Magarini kuna wahanga wapatao 2,500 kutoka Tana Delta, na sasa shirika la msalaba mwekundu nchini humo limezindua mpango wa siku tatu wa kuwasajili wakimbizi halali, na idadi ya wanafunzi wanaoweza kuendelea na masomo.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Msako wa polisi mtaa wa Eastliegh, Nairobi wakosolewa vikali -VOA Mitaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
08.04.2014
wakazi wa Eastliegh nairobi , wanalalamika kwamba polisi wanawanyanyasa na kuwabughudhi wanapoendelea na msako wa kuwasaka magaidi kufuatia mashambulizi ya karibuni nairobi.