Jumatatu, Januari 26, 2015 Local time: 01:17

Habari / Afrika

Serikali ya Tanzania yakiri elimu finyu imechangia mzozo wa gesi Mtwara

Maandamano ya wakazi wa Mtwara katika suala la uchimbaji gesi Mkoani humo
Maandamano ya wakazi wa Mtwara katika suala la uchimbaji gesi Mkoani humo
Mgogoro wa gesi asilia mkoani Mtwara nchini Tanzania bado unagonga vichwa vya wanasiasa wakati Waziri Mkuu nchini humo Mizengo Pinda akizungumzia kusudio la kutoa taarifa bungeni  juu ya muafaka uliofikiwa ili kuona kama bado ipo haja kwa bunge kuendelea kuunda tume maalum ya kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo.

Ripoti ya Dina Chahali, Dar Es Salaam
Ripoti ya Dina Chahali, Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Taarifa ya bwana Pinda imekuja siku moja tu baada ya spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Anne Makinda kuliambia bunge azma ya kuunda tume maalum  ya kwenda mkoani Mtwara kusikiliza na kutafuta ufumbuzi wa mgogoro huo wa gesi.
 
Katika mkutano wake na wandishi wa habari mjini Dodoma uliozungumzia jitihada alizofanya kulitafutia ufumbuzi suala la mgogoro wa gesi,  Waziri Mkuu amekiri kwamba tatizo kubwa lililozua mgogoro huo ni kwamba wananchi wa mkoa huo hawakupewa elimu ya kutosha juu ya utekelezaji wa mradi wenyewe wa gesi.
 
Bwana Pinda amewataka viongozi wa ngazi zote katika mkoa wa Mtwara  kuwashirikisha wananchi katika kila hatua ya mradi wa uchimbaji wa gesi hiyo asilia ili wananchi hao waweze kunufaika na fursa za mradi huo.

Katika ziara yake mkoani humo Waziri Mkuu amewahakikishia wananchi hao kuwa kiwanda cha kusafisha gesi ghafi kitajengwa mjini Mtwara, kwa hiyo hawana budi sasa kujipanga vyema kuzitumia fursa zitakazojitokeza kupitia mradi huo mkubwa.
 
Wakati huo huo Waziri wa mambo ya ndani ya nchi  Bwana Emmanuel Nchimbi amewataka wananchi kuelewa kwamba uharibifu wa mali za serikali wakati wa vurugu ni hasara yao kwavile mali hizo zimewekwa hapo kupitia kodi zao mbalimbali.
 
Alisema vurugu zilizotokea katika maeneo ya mtwara mjini na wilayani Masasi, tathimini ya awali inaonyesha kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imepata hasara ya mali zenye thamani ya shilingi bilioni 1.5  na ili halmashauri hiyo iweze kurejea kufanya kazi zake, kiasi cha shilingi milioni 791 zinahitajika.
 
 • Rais Jakaya Kikwete amkaribisha Rais Joseph Kabila Dar-es-Salaam
 • Rais Joseph Kabila apokelewa Dar es Salaam
 • Rais Jakaya Kikwete na Rais Joseph Kabila wakitumbwizwa na wanamuziki
 • Rais Jakaya Kikweti wa Tanzania na Rais Kabila wa DRC wakaribishwa na ngoma za kiyenyeji
 • rais Jakaya Kikwete wa Tanzania (kulia) na Rais Joseph Kabila wa DRC (kushoto) waelekea Ikulu
Katika habari nyingine jijini Dar Es Salaam, Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo-DRC  aliwasili nchini kwa ziara ya siku moja ambapo atakuwa na mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete. Rais Kikwete ni mwenyekiti wa asasi ya ulinzi na usalama ya jumuiya ya maendeleo ya kusini mwa afrika-SADC kitengo kinachoshughulikia pia mgogoro wa kisiasa mashariki mwa Congo.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Tatizo la maji, Pwani, Tanzaniai
|| 0:00:00
...  
🔇
X
20.01.2015 18:50
Tatizo la maji safi linavyohangaisha wananchi katika maeneo ya mkoa wa Pwani, Tanzania. Vijiji hivi viko chini ya maili 50 tu kutoka mji mkubwa wa biashara, Dar es Salaam.