Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 06:12

Sejusa afunguliwa mashitaka, Uganda.


Jenerali Sejusa akiwasili mahakamani
Jenerali Sejusa akiwasili mahakamani
Aliyekuwa mkuu wa ujasusi nchini Uganda na ambaye sasa ni mkosoaji mkubwa wa Rais Yoweri Museveni, Jenerali David Sejusa, amefikishwa katika mahakama ya kijeshi jijini Kampala Jumanne,na kufunguliwa mashtaka matatu.
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:14 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Jenerali David Sejusa, mwenye umri wa miaka 61, amefunguliwa mashtaka matatu yakiwemo kushiriki mikutano ya kisiasa kinyume cha sheria za jeshi la Uganda UPDF, kutofika kazini bila idhini pamoja na kutomtii mkuu wa majeshi.

Katika taarifa yake ya ufunguzi Jenerali Sejusa alisema hana tatizo kwa kesi yake kusikilizwa na wadogo wake licha ya kuwa ni kinyume cha sheria ya jeshi la nchi hiyo.
Jenerali David Sejusa akitoka mahakama ya kijeshi
Jenerali David Sejusa akitoka mahakama ya kijeshi
Mkuu huyo wa zamani wa ujasusi alikataa kukubali kama anakosa au la akisema, msimamo wake ni kwamba kuna kesi inayohusiana na hiyo mbele ya mahakama kuu ya nchi, na hivyo anataka sheria iheshimiwe.
Hakimu baada ya saa nne ya kusikiliza kesi aliamuru Jenerali Sejusa kupelekwa na kuwekwa katika jela yenye usalama mkubwa hadi kesi itakaposikilizwa tena wiki ijayo.
XS
SM
MD
LG