Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 01:23

Jaji Scalia wa Marekani afariki


Jaji Antonin Scalia
Jaji Antonin Scalia

Jaji wa mahakama kuu ya Marekani Antonin Scalia, amefariki dunia. Alikuwa jaji wa muda mrefu kuliko wote katika mahakama kuu ya Marekani.

Scalia alifariki usingizini katika kilichoelezwa kuwa lifo cha kawaida katika shamba la Cibolo Creek, eneo la mapumziko kaskazini-magharibi ya jimbo la Texas.

Scalia ambaye alikuwa mkonsevativu katika mahakama hiyo alikuwa na umrti wa miaka 79. Alichaguliwa kuwa jaji wa mahakama na Rais Ronald Reagan mwaka 1986.

Ikulu ya Marekani - White House - inasema Rais Barack Obama ametuma salamu za rambi rambi kwa familia ya Jaji Scalia na anatazamiwa kutoa matamshi ya kina baadaye.

Jaji Mkuu John Roberts, akithibitisha lifo cha Scalia, alisema "alikuwa jaji wa kipekee, aliyekuwa akichukuliwa na wenzake kama hazina kubwa."

Kifo cha Scalia kinatoa nafasi kwa Rais Barack Obama kuteuwa jaji mwengine wa mahakama kuu kabla ya kuondoka madarakani.

XS
SM
MD
LG