Jumanne, Mei 26, 2015 Local time: 02:24

Habari / Marekani

Romney abadilisha kauli yake juu ya bima ya afya

Asema kama ilivyo kwenye "Obamacare", yeye atahakikisha kuwa wale wenye hali ya magonjwa sugu watakuwa bado na uwezo wa kuhudumiwa kibatibabu

Mitt Romney, mgombea kiti cha nafasi ya rais Marekani kupitia chama cha Repuplican
Mitt Romney, mgombea kiti cha nafasi ya rais Marekani kupitia chama cha Repuplican
Mgombea nafasi wa kiti cha rais kwa chama cha Repuplican, Mitt Romney amebadili nia sasa na kusema hatobadilisha baadhi ya vipengele vya mpango wa huduma ya afya ulioidhinishwa na Rais Barack Obama, licha ya ahadi zake za hapo awali za kufuta kabisa sheria ya mfumo mzima wa afya ulioidhinishwa na bwana Obama, endapo atachaguliwa kuwa Rais wa Marekani mwezi Novemba.

Bwana Romney alisema hayo kwenye kipindi cha “Meet the Press” kinachorushwa na kituo cha televisheni ya ABC nchini Marekani hapo Jumapili akiongeza kuwa sasa anapanga kuutathmini tena mpango huo unaojulikana sana kama “Obamacare” na kuutathmini upya  mpango anaopendekeza mwenyewe.
 
Lakini alielezea kwa kina kuwa   kama ilivyo kwenye  mpango wa Rais  Obama, atahakikisha kuwa wale wenye hali ya magonjwa sugu watakuwa bado na uwezo wa kuhudumiwa kimatibabu na kwamba vijana wataweza kuendelea kubaki kwenye bima ya afya za wazazi wao hadi wafikie umri wa miaka 26.
 
Alielezea kwamba wakati alipokuwa gavana katika jimbo la Massachusetts, mpango wake wa afya ulikuwa na vipengele hivyo.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.