Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:02

Ripoti yasema CIA iliwatesa wafungwa


Mwenyekiti wa kamati ya ujasusi wa baraza la Seneti, Marekani, Dianne Feinstein akisoma ripoti hiyo Jumanne, Desemba 9, 2014.
Mwenyekiti wa kamati ya ujasusi wa baraza la Seneti, Marekani, Dianne Feinstein akisoma ripoti hiyo Jumanne, Desemba 9, 2014.

Ripoti ya kamati ya upelelezi ya baraza la Seneti imesema idara ya Ujasusi ya Marekani CIA iliwatesa watuhumiwa wa ugaidi kufuatia mashambulizi ya ugaidi ya Septemba 11 mwaka 2001 wakati ikifanya mahojiano ambapo ilikuwa kinyume na thamini za Marekani.

Kamati ya Seneti imetoa ripoti hiyo Jumanne kuhusu namna CIA ilivyofanya mahojiano, na kusema idara hiyo ya ujasusi haiku watendea haki wafungwa waliokuwa wanashutumiwa kwa ugaidi.

Ripoti hiyo pia imesema CIA ilipotosha Bunge na watu wa Marekani kutowapatia taarifa sahihi ya ufanisi wa mbinu zilizotumika zikiwemo kuwaweka wafungwa kwenye sehemu ndogo, kuwanyima usingizi, na kuwazamisha kwenye maji.

Akitoa ripoti hiyo, Seneta Dianne Feinstein amesema chini na jina lolote ambalo CIA ilitumia, washukiwa hao waliteswa.

“Inaonyesha kwamba matendo ya CIA miaka kumi iliyopita yanatia doa maadili yetu na historia yetu,” alisema Feinstein wakati akisoma ripoti hiyo.

Alipoingia madarakani mwaka 2009, Rais Barack Obama alipiga marufuku kutumika kwa kile kilichoitwa mbinu za hali ya juu za mahojiano ambazo zilipitishwa na Rais aliyepita George W. Bush baada ya mashambulizi ya 2001 ambayo yaliua karibu watu 3,000.

XS
SM
MD
LG