Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:59

Rais wa Cuba afanya ziara rasmi Ufaransa


Rais wa Cuba Raul Castro akianza ziara yake ya kwanza rasmi ya kitaifa nchini Ufaransa
Rais wa Cuba Raul Castro akianza ziara yake ya kwanza rasmi ya kitaifa nchini Ufaransa

Waziri wa Nishati wa Ufaransa, Segolene Royal alimkaribisha kiongozi wa Cuba kwenye uwanja wa mapinduzi ya Ufaransa mjini Paris.

Rais wa Cuba, Raul Castro ameanza hii leo ziara yake ya kwanza rasmi ya kitaifa nchini Ufaransa, ingawa aliwasili nchini humo tangu Jumamosi. Waziri wa Nishati wa Ufaransa Segolene Royal alimkaribisha kiongozi huyo wa Cuba kwenye uwanja wa mapinduzi ya Ufaransa mjini Paris.

Rais wa Ufaransa Francois Hollande anatarajiwa kumuandalia Castro mwenye umri wa miaka 84 dhifa ya jioni kwenye ikulu ya Elysee baadaye leo. Hollande ndiye kiongozi wa kwanza kutoka Ulaya kutembelea Cuba baada ya kisiwa hicho kurejesha uhusiano wa kidiplomasia na Marekani. Rais Hollande amesema kuwa ziara ya Castro ni awamu mpya katika kuimarisha uhusiano baina ya mataifa yote mawili.

Ziara ya Castro imefanyika miezi michache tu baada ya wakopeshaji wa kimataifa wa kundi linalojulikana kama Paris Club kufuta deni la dola bilioni 8.5 lililokuwa linadaiwa Cuba. Ufaransa ndio iliongoza juhudi za kufuta deni hilo.

XS
SM
MD
LG