Alhamisi, Septemba 18, 2014 Local time: 19:42

Habari / Marekani

Rais Obama kuliwaza familia Newtown

Mourners grieve at one of the makeshift memorials for victims of the Sandy Hook Elementary School shooting, December 16, 2012, in Newtown, Conn. Mourners grieve at one of the makeshift memorials for victims of the Sandy Hook Elementary School shooting, December 16, 2012, in Newtown, Conn.
x
Mourners grieve at one of the makeshift memorials for victims of the Sandy Hook Elementary School shooting, December 16, 2012, in Newtown, Conn.
Mourners grieve at one of the makeshift memorials for victims of the Sandy Hook Elementary School shooting, December 16, 2012, in Newtown, Conn.
Rais wa Marekani Barack Obama Jumapili atakwenda Newtown, jimbo la Connecticut  kuliwaza  wakazi wa mji uliokumbwa na msiba mkubwa baada ya mshambuliaji kuuwa watoto 20 wa shule ya Sandy Hook  pamoja na watu wazima sita.

White House imesema rais Obama  atakutana na familia za waliopoteza wapendwa wao na pia kuwashukuru wote waliokwenda shuleni humo kusaidia waathiriwa wa mkasa huo.  Bw. Obama  atazungumza  Jumapili jioni kwenye  mkusanyiko wa watu wanaomboleza  pamoja na familia za waathiriwa.

Polisi wa Connecticut wamewatambulisha waliouawa  wakiwemo wasichana 12 na wavulana wanane  wote wa kati ya umri wa miaka 6 na 7.Watu wazima wote sita waliouawa walikuwa wanawake.

Afisa wa afya aliyekagua maiti zao alisema wote walipigwa risasi wakiwa hatua chache kutoka kwa muuaji huyo kabla hajajiuwa kwa risasi.  Msiba huu wa kihistoria Marekani umegonga vichwa vya habari Marekani na nchi za Ulaya na bara Asia.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Mgomo wa Wafanyabiashara Dar es Salaam - VOA Mitaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
03.09.2014 16:46
Baadhi ya wafanyabiashara wa Dar es Salaam wamefanya mgomo kupinga utumiaji wa mashini za elektroniki zaa kutoa risiti, kuweza kupima mapato yao kwa ajili ya kodi EFD.