Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 00:49

Rais Mugabe ateuliwa kuwa mwenyekiti wa AU


Viongozi wa Umoja wa Afrika, Addis Ababa Ethiopia Januari 30,2015
Viongozi wa Umoja wa Afrika, Addis Ababa Ethiopia Januari 30,2015

Viongozi hao wa Afrika, wakiongozwa na rais wa Uganda Yoweri Museveni pia watajadilia mkakati wa kujiondoa kwenye uwanachana wa Mahakama ya Kimataifa ya jinai-ICC.

Viongozi wa Umoja wa Afrika wamemteua rais Robert Mugabe wa Kiongozi huyu mwenye miaka 90 amekabidhiwa wadhifa huo na Rais wa Mauritania ,Mohamed Ould Abed Aziz ambaye alikuwa mwenyekiti hapo awali.

Viongozi hao wa Afrika, wakiongozwa na rais wa Uganda Yoweri Museveni pia watajadilia mkakati wa kujiondoa kwenye uwanachana wa Mahakama ya Kimataifa ya jinai-ICC.

Akizungumza na waandishi habari hapo awali jijini Nairobi, rais huyo wa Uganda alisema “Mahakama hiyo ya Wazungu inaendelea kuonyesha ujeuri na dharau kwa Waafrika.” Alisema ingawa ICC imeondoa kesi dhidi ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, bado hajaridhika kwa sababu kesi dhidi ya Naibu rais wa Kenya William Ruto ingali inaendelea.

Wakati huo, huo viongozi hao wa Afrika wameidhinisha mpango wa kupeleka kikosi cha pamoja cha wanajeshi 7,500 cha kukabiliana na wanamgambo wa Boko Haram.

Hatua hiyo imefikiwa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Afrika uliofanyika Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia Ijumaa . Nchi za Nigeria , Cameroon,Chad, Niger na Benin zilikubaliana kushirikana katika juhudi za kukabiliana na wanamgambo hao ambao wameua maelfu ya raia huko Nigeria na kujinyakulia eneo kubwa la jimbo la Borno karibu na mpaka wa Cameroon na Chad.

XS
SM
MD
LG