Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 21:03

Polisi Malawi watumia gesi ya machozi kutawanya waandamanaji


Rais Joyce Banda aliposhiriki kwenye upigaji kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 20, 2014
Rais Joyce Banda aliposhiriki kwenye upigaji kura katika uchaguzi mkuu uliofanyika Mei 20, 2014
Polisi nchini Malawi wamefyatua gesi ya kutoa machozi kuwasambaratisha waandamanaji wanaodai kuhesabiwa tena kura za uchaguzi wa rais zilizopigwa wiki iliyopita.

Waandamanaji walichoma matairi na waliharibu maduka Ijumaa katika mji mkuu Lilongwe kabla ya kilichotarajiwa na mahakama kuu nchini humo kutangazwa kama matokeo ya uchaguzi uliokuwa na mzozo yatatolewa hadharani au kura zitarudiwa kuhesabiwa.

Uchaguzi uligubikwa na matatizo yakiwemo kuchelewa kufunguliwa kwa vituo vya kupiga kura na kasoro nyingine kwenye karatasi za uchaguzi. Matatizo hayo yalichochea tume ya uchaguzi nchini humo kuongeza muda wa kupiga kura kwa siku moja zaidi na kisha siku ya tatu upigaji kura ulifanyika kwenye baadhi ya maeneo.

Wakati huo huo Rais Joyce Banda anasema uchaguzi uligubikwa na wizi mkubwa ikiwemo wizi wa kuongeza kura katika masanduku ya kupigia kura na watu kupiga kura zaidi ya mara moja.

Aliagiza uchaguzi mpya ufanyike ndani ya muda wa siku 90 na alisema hatokuwa mgombea katika duru hiyo ya upigaji kura. Lakini mahakama kuu ilipuuzia matamshi yake wakati chama kikuu cha upinzani kilipolalamika.
XS
SM
MD
LG