Jumanne, Aprili 28, 2015 Local time: 03:29

Habari / Afrika

Polisi wanne wajeruhiwa kutokana na shambulio la gruneti Mombasa

Ghasia mjini Mombasa baada ya kuuliwa kwa Imam Aboud Rogo
Ghasia mjini Mombasa baada ya kuuliwa kwa Imam Aboud Rogo

Multimedia

Audio
Baada ya siku kamili ya utulivu katika mji wa Mombasa, polisi walokuwa wanapiga doria kati kati ya mji walishambuliwa na gruneti lililotupwa na vijana wawili walokuwa wanatembea kwa miguu.

Kufuatana na mwandishi wa Sauti ya Amerika Josphate Kioko aliyewasili katika eneo la shambulio ni kwamba mkuu wa Idara ya Ujasusi wa Mkoa wa Pwani Amros Munyasia, aliwasili mara moja na kuzungumza na waandishi habari.

Bw Munyasia anasema, wameweza kumkamata mmoja kati ya watu wawili wanaoamini walihusika na shambulio hilo na kwamba maafisa wanne wanatibiwa hospitali lakini mmoja kati yao yuko katika hali mahtuti.
Kioko azungumzia mripuko wa gruneti
Kioko azungumzia mripuko wa grunetii
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Shambulio hilo la Jumatano magharibi linatokea baada ya waziri mkuu Riala Odinga kutembelea Mombasa na kusema kwamba anaamini kuna watu walojificha walohusika na ghasia hizo.

"Nia yao ni kuwagawa wakazi wa Mombasa kati ya Wakristo na waislamu kwa lengo la kuzusha mgogoro wa kidini." alisema Raila.

Hata hivyo Raila akizungumza na waandishi habari alikata kueleza ni watu gani anaewadhania kuhusika na ghasia hiyo, akisema tu ghasia kuzuka mara tu baada ya kuuliwa kwa Imam Aboud Rogo inaashiria kulikuwepo na mpango mkubwa zaidi.

Kwa upande wake mbunge wa Mombasa Najib Balala aliyekuwa mshirika wa zamani wa Raila anasema haamini kuna ugomvi wa kidini huko Pwani bali na makundi ya wahuni wanaotumiwa kuzusha ghasia hizo.
Mahojiano na Najib Balala
Mahojiano na Najib Balalai
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Mwanaharakati mtetezi wa masuala ya haki za binadam mjini Mombasa Abu Islam akizungumza na Sauti ya Amerika anasema anamini mauwaji ya Rogo inatokana na mauwaji ya kiholele yanayoendelea huko Kenya kwa ujumla.

"Ikiwa wewe ni tishio kwa watu fulani au kwa baadhi ya watu fulani ikiwa tisho la kihaki au tisho lolote wewe unamalizwa hapo hapo," amesema Abu Islam.
Abu Islam afafanua ghasia za Jumatatu
Abu Islam afafanua ghasia za Jumatatui
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Sheikh Balala ametoa wito kwa serikali kudfanya uchunguzi wa kina na wa haraka kuweza kujuwa walohusika na mauwaji ya Imam Rogo na samir Khan ambae maiti yake iliguduliwa upande wa Voi.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Mbio za Boston Marathon, April 20, 2015i
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.04.2015 00:06
Mwanadada wa Kenya Caroline Rotich aliibuka mshindi wa mbio ndefu za Boston Marathon upande wa wanawake na Lelisa Desisa wa Ethiopia alirudia ushindi wake wa mwaka jana kwa kushinda mbio za wanaume siku ya Jumatatu April 20.