Alhamisi, Oktoba 02, 2014 Local time: 02:20

Habari / Afrika

Polisi 30 wauwawa kaskazini mwa Kenya

Polisi wasiopungua 30 wameuwawa huko Baragoi, Kenya
Polisi wasiopungua 30 wameuwawa huko Baragoi, Kenya
Watu wenye silaha huko kaskazini mwa Kenya wamewauwa maafisa polisi wasiopungua 30 ambao walikuwa wakiwasaka wezi wa mifugo.

Polisi nchini Kenya wanasema maafisa hao walishambuliwa ghafla jumamosi wakati gari lao lilipokuwa likielekea kwenye eneo moja la kaskazini katika  wilaya ya Baragoi.

Timu za uchunguzi na uokozi ziligundua miili 11 siku ya jumamosi na miili 19 mingine siku iliyofuata. Watu tisa walionusurika na shambulizi hilo wamelazwa hospitali.

Hakuna mtu yeyote aliyedai kuhusika na shambulizi hilo. Polisi wanashuku wezi wa mifugo walihusika na shambulizi jingine huko Baragoi mwezi uliopita ambalo liliuwa watu 13.

Wizi wa mifugo na ghasia zinazohusiana na hilo zinatokea mara kwa mara huko kaskazini mwa Kenya lakini mashambulizi ya moja kwa moja kwa polisi ni nadra sana.
 
Maafisa wa serikali walisema wameshtushwa na mauaji hayo na walielezea wasi wasi kuhusu maandalizi na uwezo wa majeshi ya usalama.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Maudhui ya wavuvi wa Bagamoyo-VOA Mitaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
20.09.2014 15:14
Wafanyabiashara wa samaki katika wilaya ya Bagamoyo, Tanzania waelezea changamoto zinazowakabili katika biashara kuu ya uvuvi, miongoni mwao ukosefu wa soko na mahala ya kuhifadhi samaki wanaovua.