Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 15:30

Wakenya wasubiri kwa hamu kumpokea Papa Francis


Msichana ameshika karatasi ya sala yenye picha ya Papa Francis wakati wa misa maalum kwenye kanisa la St. Joseph kwenye eneo la Kangemi katika mji mkuu Nairobi.
Msichana ameshika karatasi ya sala yenye picha ya Papa Francis wakati wa misa maalum kwenye kanisa la St. Joseph kwenye eneo la Kangemi katika mji mkuu Nairobi.

Mitaa inafanyiwa ukarabati, mabango yamebandikwa kwenye barabara kuu, na bidhaa mbali mbali zenye sura ya baba mtakatifu Francis vinauzwa. Yote haya ni kumkaribisha papa wakati atakapoanza ziara yake ya Afrikam, kituo chake cha kwanza kikiwa nchini kenya.

Kennedy Agesa ni mshoni anayeishi katika eneo la mabanda la Kangemi mjini Nairobi.

“Tumesikia uvumi kuwa baba mtakatifu anakuja, tuna furaha kubwa,” anasema Agesa.

Papa Francis atatembelea eneo la Kangemi wakati wa ziara yake. Ni mtetezi wa maskini na imekuwa ndiyo ujumbe wake mkuu katika upapa. Katika eneo lake la asili anakotokea Argentina anatajwa kuwa ni askofu wa maeneo ya mabanda.

please wait

No media source currently available

0:00 0:03:07 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Padri Simon Peter Kamomoe ni mkuu wa kanisa la Holy Family Minor Basilica mjini Nairobi. Anasema baba mtakatifu ni mtu sahihi kuzungumzia umaskini.

“Wakenya wengi, idadi kubwa ya wakenya, wanapitia kipindi kigumu, kwahiyo wanapomuona baba mtakatifu hivi sasa anaishi maisha ya kawaida, na anajitambulisha na maskini, na watu wanaopata shida,” anasema Padri Kamomoe.

Papa Francis anatarajiwa kuzungumza na vijana wa Kenya wakati wa ziara yake, na kama ziara hii itakuwa kama zile za awali, huenda akawasihi kufanya kazi pamoja, kuwa na ndoto kubwa, na zaidi ya hapo kuwa na matumaini.

Baba mtakatifu anatarajiwa kuzungumzia mabadiliko ya hali ya hewa, awali amesema kuwa watu walio katika hali duni ndiyo waaathirika wakuu.

Shirika la hisani la kanisa katoliki nchini Kenya na mwakilishi wa Somalia, Lane Bunkers anasema mabadiliko ya hali ya hewa ni hatari kwa wale ambao wanaishi kwa kutegemea kilimo.

“Pale ambapo kuna mwenendo wa mabadiliko makubwa ya hali ya hewa, pale ambako kuna misimu isiyo ya kawaida ya ukame au mvua nyingi, hii ina athari kubwa kwa mkulima mdogo,” anasema Bunkers.

Papa Francis pia atakutana na viongozi wa imani mbali mbali za dini, ikiwa ni ishara muhimu katika nchi ambayo imewahi kukumbwa na ghasia za kidini na kikabila.

Papa atakuwa kwa ziara ya siku tatu nchini Kenya kabla ya kuelekea kituo chake cha pili Uganda.

XS
SM
MD
LG