Jumatatu, Machi 30, 2015 Local time: 17:10

Habari / Afrika

Marekani yalaani mauaji wa Padri Mushi

Askofu Mkuu wa Tanzania Kardinali Pengo azungumzia kifo cha Mushii
|| 0:00:00
...  
🔇
X
18.02.2013 18:36
Kardinali Pengo atowa wito wa umoja Tanzania baada ya kuuliwa kwa Padri Mushi huko zanzibar

Tukio la kuuawa kwa kupigwa risasi padre wa kanisa Katoliki visiwani Zanzibar Jumapili na matukio mengine ya mauaji na vurugu zinazohusiana na dini, vimeelezwa kwamba vinaweka reheni amani na usalama wa nchi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo juu ya mauaji ya Paroko wa Kanisa Katoliki Minara Miwili Zanzibar, Evarist Mushi , Askofu Mkuu wa jimbo kuu  katoliki la Dar es salaam, Polycarp Kardinali Pengo, amesema  "mauaji hayo si pigo kwa kanisa Katoliki pekee bali ni pigo kwa mustakabali wa amani ya Tanzania wakati huu ambapo inashuhudiwa mauaji ya kihusisha imani za kidini."

Akikumbusha pia tukio la kunusurika kuuwawa kwa padre mwingine wa kanisa katoliki aliyepigwa risasi visiwani humo hivi karibuni.

Ripoti ya Dinah Chahali
Ripoti ya Dinah Chahalii
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Hata hivyo Polycarp Kardinali Pengo alitupia lawama vyombo vya ulinzi na usalama huko Tanzania, kutokana na kile alichodai kushindwa kudhibiti vitendo vya kihalifu na mauaji vinavyochochewa kwa misingi ya kidini.

Kwa upande wake Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema amewataka watanzania kuwa na subra wakatio huu ambapo timu maalum ya jeshi hilo imetumwa visiwani zanzibar kushughulikia tukio hilo la mauaji.

Rais Jakaya kikwete naye kupitia kurugenzi ya mawasiliano Ikulu ameagiza kuwepo uchunguzi wa haraka wa tukio hilo la mauaji ya paroko wa kanisa Katoliki.  Padre aliyeuawa  Evarist Mushi, anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano Febuari 20 , katika makaburi ya Kitope yaliyopo nje ya mji wa Zanzibar.
 
Wiki iliyopita  vurugu za kidini huko Geita pia zilisababisha mauaji ya Mchungaji Mathayo Kachila  wa Kanisa la Tanzania Assemblies Of God katika mgogoro wa kuchinja nyama.

Wakati huo, huo Marekani imelaani vikali mauaji yasiyo na msingi ya Padre Evaristus Mushi wa Zanzibar. Taarifa iliyotolewa na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania inasema mauaji hayo ya kikatili ni ya tatu kufanyika  na kulenga viongozi wa kidini visiwani Zanzibar tangu Novemba mwaka jana ambayo yanakiuka pia thamani, utamaduni na amani ya Zanzibar, kisiwa kinachojulikana kwa utajiri wa kitamaduni, kustahamiliana.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba Ghasia za kidini hazina nafasi Tanzania au kwingineko. Marekani inasimama kama mshirika mkuu wa raia wote wa nchi hiyo na inatoa wito kwao kuendelea kupinga ghasia zinazofanywa na wale wanaotaka kuhujumu  usalama wa raia wenzao.
mjadala huu umefungwa
Comment Sorting
Maoni
     
Na: jackson majuto Kutoka: moshi kilimanjaro
19.02.2013 19:20
jaman wazanzibar mbona mnataka kuitumbukiza nchi katka vita vya kidin? kumbukeni kuvuruga aman ni tendo la siku 1 tu ila kuirudsha ni zaid ya miaka 100

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Waandamana kupinga ubakaji Kenyai
|| 0:00:00
...  
🔇
X
27.03.2015 18:06
Mamia ya wanawake nchini Kenya hivi majuzi walishiriki maandamano kupinga vitendo vya ubakaji ambayo vimekithiri nchini humo