Jumapili, Aprili 19, 2015 Local time: 20:32

Habari / Afrika

Oscar Pistorius apanda kizimbani

Oscar Pistorius akiwa kwenye michuano ya Olympic mjini LondonOscar Pistorius akiwa kwenye michuano ya Olympic mjini London
x
Oscar Pistorius akiwa kwenye michuano ya Olympic mjini London
Oscar Pistorius akiwa kwenye michuano ya Olympic mjini London
Mwanariadha wa Afrika Kusini katika michuano ya Olympic Oscar Pistorius alikuwa kwenye mahakama moja ya Pretoria Jumanne ambapo anakabiliwa na mashtaka ya mauaji kwa kumfyatulia risasi na kumwua rafiki yake wa kike, mrembo Reeva Steenkamp. Pistorius atakabiliwa na mapambano makali ya kupata dhamana baada ya jaji kusema  kuwa aliyapanga mauaji hayo.
 
Mwendesha mashtaka mkuu Gerrie Nel hakusema chochote wakati wa kusikilizwa  kesi hiyo , akitangaza kuwa Oscar Pistorius anashtakiwa kwa mauaji. Tangazo hilo limepelekea mwanariadha huyo wa michuano ya Olympic kulia.

Nel kisha alielezea mtazamo wa mauaji yaliyotokea Februari 14 kwenye nyumba ya Pistorius huko Pretoria.

Picha aliyochora ilikuwa kielelezo:  Mlemavu huyo wa miguu yote miwili alishutumiwa kuambatanisha viungo vyake bandia, alitembea mita saba kuelekea karibu na bafu na kumfyatulia risasi mara nne Reeva Steenkamp kupitia mlango ambao ulikuwa umefungwa. Nel aliiambia mahakama kwamba Pistorius kisha alivunja mlango kutoka nje na kuubeba mwili wa mpenzi wake hadi chumba cha chini na alimuita rafiki mmoja  akimweleza  kuwa alidhani Steenkamp alikuwa mwizi.
 
Dai hilo Nel alisema linaonyesha kwamba Pistorius alipanga mauaji.
Mwendesha mashtaka Desmond Nair alikubali akisema  hakuna shaka yalikuwa mauaji ya kukusudia.
 
Wakili wa utetezi Barry Roux aliangalia mtazamo tofauti  akielezea  kuwa hayo si mauaji.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Mgomo wa mabasi ya abiria Tanzania VOA MItaanii
|| 0:00:00
...  
🔇
X
10.04.2015 19:18
Mgomo wa madereva ya basi za umaa Tanzania umesababisha usumbufu mkubwa kwa abiria kote nchini.