Jumatatu, Septemba 22, 2014 Local time: 10:12

Radio / Michezo

Afrika Kusini, Cape Verde kufungua dimba Jan 19

Uwanja wa mpira Johannesburg ambapo baadhi ya mechi za fainali ya kombe za Afrika zitafanyika mwakani. Uwanja wa mpira Johannesburg ambapo baadhi ya mechi za fainali ya kombe za Afrika zitafanyika mwakani.
x
Uwanja wa mpira Johannesburg ambapo baadhi ya mechi za fainali ya kombe za Afrika zitafanyika mwakani.
Uwanja wa mpira Johannesburg ambapo baadhi ya mechi za fainali ya kombe za Afrika zitafanyika mwakani.
Wenyeji Afrika Kusini na Cape Verde zitachuana katika mechi ya ufunguzi wa fainali za kombe la mataifa Afrika hapo Januari 19, 2013 nchini Afrika Kusini. Ratiba ya makundi ilitangazwa nchini humo Jumatano usiku katika sherehe ambazo zilihudhuriwa pia na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma.

Ratiba ya makundi inaonyesha kuwa wenyeji Afrika Kusini watakuwa katika kundi A pamoja na Cape Verde, Angola na Morocco. Kundi B litakuwa na nchi za Ghana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Niger na Mali wakati mabingwa watetezi Zambia, Nigeria, Ethiopia na Burkina Faso watachuana katika kundi C. Kundi D litajumuisha timu za mataifa ya Ivory Coast, Togo, Algeria na Tunisia.

Wachambuzi wa kandanda wanasema jinsi makundi hayo yalivyojitokeza katika fainali hizo hakuna kundi ambalo linaweza kusemwa kwa uhakika kuwa "kundi la kifo" kwani timu kubwa kama vile Ghana, Nigeria, Ivory Coast and wenyeji Afrika Kusini zote ziko katika makundi tofauti

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Maudhui ya wavuvi wa Bagamoyo-VOA Mitaanii
|| 0:00:00
...
 
🔇
X
20.09.2014 15:14
Wafanyabiashara wa samaki katika wilaya ya Bagamoyo, Tanzania waelezea changamoto zinazowakabili katika biashara kuu ya uvuvi, miongoni mwao ukosefu wa soko na mahala ya kuhifadhi samaki wanaovua.