Jumatano, Machi 04, 2015 Local time: 09:56

Habari / Afrika

Odinga na Musyoka waungana 2013

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga
Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga
Mahasimu wakuu wa kisiasa nchini Kenya, Waziri Mkuu Raila Odinga na Makamu Rais, Kalonzo Musyoka, Jumanne jioni walitia saini makubaliano ya kushirikiana kwenye uchaguzi mkuu ujao na hatimaye kuunda serikali ya muungano.

Hii ni mara ya pili kwa viongozi wa kisiasa nchini Kenya kutia saini makubaliano ya kushirikiana kwenye kampeni ya uchaguzi mkuu  unaotarajiwa kufanyika mwezi Machi mwakani.

Na Mwai Gikonyo, Nairobi
Na Mwai Gikonyo, Nairobii
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Katika sherehe zilizohudhuriwa na watu mbali mbali kwenye ukumbi wa mikutano wa  kimataifa wa Kenyatta mjini Nairobi, bwana Odinga na bwana Musyoka, pia walimshirikisha kiongozi wa chama cha FORD Kenya, Moses Wetangula ambaye pia ni waziri wa biashara. Vile vile kuna vyama vya kisiasa vingine 11 vilivyoshirikishwa katika makubaliano hayo lakini baadhi yake ni vyama vya watu binafsi.
 
Akizungumza katika sherehe hizo Musyoka alisema hisia zake za kisiasa sasa zimebadilika kumhusu Raila Odinga “ kama ningekuwa mtu wa kushikilia ghadhabu hasira nisingekuwa hapa leo na mheshimiwa Odinga lakini tunasema hayo sasa iko nyuma yetu ni lazima tuyagange yaliyo mbele ili vile dada yetu Ngilu amesema juu ya shida ya wananchi kutokuwa na kazi kutokuwa na ajira wananchi kulala hoi na wengine wanalala hai”.
 
Wakati huo huo Waziri Mkuu Odinga alishutumu vikali miungano ya kisiasa inayojengwa kwenye misingi ya kikabila. Alisema “ vyama vishindane kwa sera sio kwa msingi ya ukabila ati kabila hii iungane na kabila hii inyakue utawala, nataka kuona kama mwanasiasa wako kwenye mstari wa mbele kuunganisha wakenya”.

Ikiwa imesalia takribani miezi miwili kabla ya uchaguzi kufanyika kumekuwa kumekuwa na harakati za wanasiasa kukamilisha miungano ya kisiasa kabla ya muda wa mwisho wa kuwasilisha mikataba hiyo katika ofisi ya vyama vya msajili wa kisiasa.
mjadala huu umefungwa
Comment Sorting
Maoni
     
Na: E Kutoka: mozambique
07.12.2012 12:00
sawa

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Wakenya watoa maoni kuhusu mfumo wa dijitalii
|| 0:00:00
...  
🔇
X
26.02.2015 19:55
Tangu uamuzi wa serikali kuondoa matangazo ya analog Wakenya wamekuwa na maoni tofauti kuhusu mfumo huo na kuzimwa kwa baadhi ya matangazo ya mashirika makuu ya televisheni Kenya