Jumatatu, Mei 25, 2015 Local time: 04:09

Habari / Marekani

Obama, Romney waanza kampeni kwenye majimbo muhimu

Wagombea wote, Rais Obama na mpinzani wake Romney, wanaitumia siku ya Ijumaa kuwahamasisha wapiga kura katika majimbo ya Iowa na New Hampshire

Rais Obama akiwa kwenye kampeni katika chuo kikuu cha Iowa
Rais Obama akiwa kwenye kampeni katika chuo kikuu cha Iowa
Rais wa Marekani Barack Obama ameanza siku tatu za kampeni kwenye majimbo yasiyoelekea kwa chama chochote hapo Ijumaa, siku moja baada ya kukubali uteuzi wa ugombea urais kwa chama cha Democrat.
 
Wagombea wote, Rais Obama na mpinzani wake wa m-Republican, Mitt Romney, wanaitumia siku ya Ijumaa kuwahamasisha wapiga kura katika majimbo ya Iowa na New Hampshire, majimbo mawili muhimu katika uchaguzi mkuu wa mwezi Novemba.

Alhamis  usiku Bw.Obama aliwaambia wafuasi wake kwenye mkutano mkuu wa kitaifa wa chama cha Democrat huko Charlotte, North Carolina  kuwa “wanakabiliwa na chaguo la wazi katika kizazi hiki”, pale wanapokwenda kupiga kura mwezi Novemba, “chaguo kati ya njia mbili tofauti kwa wa-marekani”.
 
Aliwataka wamarekani kujumuika pamoja  kuangalia malengo yao katika maeneo ya viwanda, nishati, elimu, usalama wa taifa na punguzo la nakisi akisema yatapelekea “kuongoza upatikanaji wa ajira mpya, nafasi zaidi na kujenga tena uchumi huu kwenye msingi imara”.

Wakati huo huo kampeni ya Romney inatangaza itatoa matangazo mapya 15 ya televisheni Ijumaa yanayolenga juu ya uchumi.
 
Katika hotuba yake ya Alhamis,Obama alikamilisha kwa kumkosoa vikali mpinzani wake Romney na chama chake cha Repuplican juu ya masuala kadhaa ikiwemo sera za nje, kodi na huduma ya afya.

Alisema kwamba wa-Repuplican wanatoa wito wa kukata kodi kama suluhisho la kila kitu.  Lakini alisema yeye haamini kuwapa nafuu ya kodi mamilionea wataleta ajira au kupunguza nakisi ya taifa. Katika suala la sera za nje, alimshutumu Romney kwa kutaka kulirudisha taifa nyuma kuelekea enzi za “majigambo na makosa” katika sera za mambo ya nje.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.