Ijumaa, Februari 12, 2016 Local time: 21:07

  Habari / Afrika

  Obama kukutana na viongozi wa Congress

  Rais wa Marekani Barack Obama
  Rais wa Marekani Barack Obama
  Rais Barack Obama wa Marekani amewaita viongozi wa bunge kwa mazungumzo huko White House wiki ijayo juu ya namna ya kuweza kukata matumizi ya serikali na ongezeko la kodi mwezi Januari.
   
  Bwana Obama ambaye alichaguliwa tena kuongoza muhula wa pili wa miaka minne aliuambia mkusanyiko huko White House kwamba nchi inahitaji haraka kujenga umoja ili kutatua matatizo yake ya kifedha, na kipaumbele cha kuhamasisha ajira na ukuaji wa uchumi.

  Bwana Obama alisema inahitajika kudhibiti matumizi ya serikali.  Lakini aliongeza kuwa hatuwezi kupata mafanikio kwa kupunguza tu matumizi katika mipango ya serikali.

  Alisema uchaguzi ulionyesha kwamba wamarekani wengi wanaidhinisha mpango wake wa kuongeza kodi kwa matajiri, familia kama zile zinazotengeneza zaidi ya dola 250,000 kwa mwaka. Wapinzani wake wa chama cha Republican bungeni wanapinga mpango wowote wa kuongeza kodi unaotakiwa kuanza mwaka mpya.

  Marekani inakabiliwa na kile Washington inachokiita “fiscal cliff” ukataji matumizi wa lazima wa dola bilioni 600 ili kuokoa program za taifa na ongezeko la kodi ambalo litawa-athiri wafanyakazi wote wa Marekani ifikapo Januari mosi.

  Wachambuzi wengi wa masuala ya uchumi wana wasi wasi wa ukataji na ongezeko la kodi, kama jambo hilo likitokea, linaweza kurudisha  hali ya uchumi kuwa mbaya.

  Awali spika wa bunge, m-Republican John Boehner aliwaambia waandishi wa habari kwamba kuongeza kiwango cha kodi kutazorotesha uwezo wa kubuni ajira ambazo kila mmoja anazitaka. Alisema suala la uchumi lilikuwa kipaumbele kwa wapiga kura katika uchaguzi mkuu uliomalizika wiki hii.
   
  Boehner alisema mwaka 2013 unatakiwa kuwa mwaka wa serikali kuanza kutatua matatizo yake ya kifedha hasa masuala ya madeni, kodi na matumizi kwa pensheni ya serikali na huduma ya afya kwa wazee.

  Boehner anasema yupo wazi kwa baadhi ya mabadiliko ya kuongeza mapato mapya ya serikali, iwapo yanajumuisha mabadiliko kwa pensheni na program za huduma ya afya.

  You May Like

  Jioni

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.
  VOA Express

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
  Alfajiri

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

  mjadala huu umefungwa
  Maoni
       
  Hakuna mtu ameandika maoni hapa. Kuwa wa kwanza kutoa maoni.