Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 16:40

Obama kukutana na viongozi 50 wa Afrika


Rais wa Marekani, Barack Obama
Rais wa Marekani, Barack Obama
White House inasema Rais wa Marekani Barack Obama atawaalika viongozi takribani 50 wa serikali za barani Afrika kushiriki mkutano wa mwezi Agosti mjini Washington.

please wait

No media source currently available

0:00 0:01:13 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Naibu msemaji wa White House, Jonathan Lalley anasema bwana Obama atawajumuisha wakuu wote wa nchi au serikali za bara la Afrika ukiwatoa wale ambao hawana uhusiano mzuri na Marekani au waliosimamishwa kwa muda uanachama na Umoja wa Afrika-AU.

Lalley anasema mwenyekiti wa AU, Nkosazana Dlamini-Zuma pia ataalikwa kwenye mkutano ambao unafanyika Agosti tano hadi sita. White House ilitangaza mkutano huo jumanne ikisema Marekani itautumia kuimarisha ushirikiano wa biashara na uwekezaji na bara la Afrika.

Maafisa wanasema bwana Obama pia anamatumaini ya kujenga mafanikio yaliyopatikana tangu ziara yake ya mwezi Juni mwaka 2013 barani afrika. White House inasema nchi ambazo zitapokea mialiko ya mkutano wa Agosti ni pamoja na Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Ethiopia, Sudan Kusini, Mali na Nigeria.
XS
SM
MD
LG