Jumatatu, Mei 20, 2013 Local time: 07:39

Habari / Marekani

Rais Barack Obama atembelea eneo lilioathiriwa na kimbunga Sandy.

Baadhi ya maeneo yalioathiriwa na kimbunga huko New York.
Baadhi ya maeneo yalioathiriwa na kimbunga huko New York.
ukubwa wa habari - +
Rais wa Marekani Barack Obama ametembelea eneo lilioathiriwa vibaya na kimbunga huko kwenye pwani New Jersey jumatano akiwaambia wakazi walioathirika vibaya kwamba serikali  kuu itawasaidia kwa mpaka mwisho .
 
Akisindikizwa na Gavana wa jimbo hilo Chris Christie Bw.Obama aliwahakikishia mamilioni ya wakazi wa New Jersey na wakazi wengi  wa jiji kuu la New York . Alitoa rambi rambi kwa  kwa familia zilizopoteza ndugu na wapendwa wao na kuahidi “tutafuatilia mpate kila msaada mnaohitaji ili kujijenga upya”.
 
Rais pia alisema makampuni ya umeme yalioko mbali na eneo hilo mpaka huko Carlifornia yameahidi kusaidia. Alisema ameagiza ndege za kijeshi kusafirisha vifaa na wafanyakazi kuelekea eneo hilo haraka iwezekanavyo.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--