Jumatatu, Novemba 24, 2014 Local time: 16:40

Habari / Marekani

Obama arudi Washington kujadili mzozo wa bajeti

Rais Barack Obama awasili Honolulu na familia yake kuanza likizo ya Krismas huko Hawaii, Jumamosi, Dec. 22, 2012.
Rais Barack Obama awasili Honolulu na familia yake kuanza likizo ya Krismas huko Hawaii, Jumamosi, Dec. 22, 2012.
Rais Barack Obama wa Marekani amefupisha likizo yake katika jimbo la Hawaii na atarudi Washington kuanza tena mazungumzo na viongozi wa bunge yanayolenga kufikia makubaliano ya kupunguza nakisi kabla ya mwaka kuisha.
 
White House inasema Rais Obama ataondoka Hawaii Jumatano na anatarajiwa kufika Washington Alhamis asubuhi.

Mwanzoni mwa wiki iliyopita rais alisema yeye na spika wa bunge m-Republican, John Boehner walikaribia kufikia makubaliano juu ya kukamilisha mtafaruku wa fedha uliopo ili kuepuka kile kinachoitwa “Fiscal Cliff” ukataji wa matumizi ya lazima ya dola bilioni 500 na ongezeko la kodi ambalo litawaathiri takribani wafanyakazi wote wa  Marekani kuanzia Januari mosi. Lakini mwishoni mwa wiki iliyopita juhudi hizo zilivurugika wakati wabunge walipoondoka Washington kwa likizo fupi ya kusheherekea sikukuu ya Krismas.
 
Bwana Obama na familia yake pia waliondoka White House na kuelekea Hawaii na kile kwa kawaida huwa likizo ndefu wakati wa sikukuu. Lakini mwaka huu Obama atarudi mapema kwa ajili ya mazungumzo ya “Fiscal Cliff”.

Likizo ya sikukuu ilianza muda mfupi baada ya wabunge wa chama cha Republican kuzorotesha jaribio la kupitisha pendekezo la suluhisho lililotolewa na Boehner ambalo litaongeza kodi kwa mamilionea huku ikipunguza kodi kwa watu wengine wa daraja la kati. Bwana Obama anataka nafuu ya kuongezewa kodi kwa kufikia kiwango cha mapato ya dola 400,000.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Usafiri wa Bodaboda Dar es Salaam - Voamitaanii
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.11.2014 08:18
Wasfiri wa Bodaboda waeleza maadhui yao na usafiri huo katika jiji la Dar Es Salaam.