Jumapili, Februari 14, 2016 Local time: 06:48

  Habari / Afrika

  Obama Amsisitiza Kagame kutowasaidia M23

  Rais wa Marekani Barack Obama
  Rais wa Marekani Barack Obama
  Rais wa Marekani Barack Obama amemsisitiza  Rais wa Rwanda Paul Kagame  umuhimu wa kusitisha kabisa uungaji mkono wowote kwa waasi katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC.

  Jopo moja la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linaishutumu Rwanda na Uganda kwa kuliunga mkono kundi la  uasi la M23 ambalo karibuni liliondoka kutoka Goma baada ya kuuteka mji huo wa mashariki mwa Congo. Wote Rwanda na Uganda wanakanusha madai hayo.

  White House inasema Obama alimsihi Kagame wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu Jumanne  kutekeleza kikamilifu ahadi zake alizotoa katika mazungumzo ya  amani  ya kieneo juu ya  kubuni  makubaliano ya kisiasa ambayo yanajumuisha kumalizika uepukaji wa sheria kwa makamanda wa M23 ambao wametenda ukiukaji mkubwa  wa haki za binadamu.

  Anasema mzozo huo ni budi umalizike  kwa makubaliano ambayo yatalinda hadhi ya kitaifa ya  DRC na kuzungumzia usalama wa kieneo pamoja na masuala ya uchumi na utawala.
   
  Wakati huo huo wizara ya fedha nchini Marekani ilitoa vikwazo vipya Jumanne dhidi ya viongozi wawili waandamizi wa kundi la M23 kwa kuwatumia watoto kama wanajeshi na harakati nyingine zinazochangia mapigano nchini DRC.

  Inasema Baudoin Ngaruye na Innocent Kaine wanahusika kwa vitendo vibaya vya ghasia na kwamba Kaine alifanya vitendo vinavyowalenga watoto kupitia mauaji, ukataji viungo vya mwili  na ghasia za ngono.

  Pia Jumanne wachunguzi wa Umoja wa Mataifa walisema ushahidi wa awali kuhusu mashitaka ya shutuma za ghasia zilizotokea mwezi uliopita huko Minova karibu na Goma zilionesha kesi 126 zilizoripotiwa za ubakaji na mauaji ya watu wawili.
   
  Msemaji wa Umoja wa Mataifa alisema uchunguzi tofauti uliofanywa na jeshi la Congo umepelekea kukamatwa kwa wanajeshi tisa wakiwemo wawili wakihusika na ubakaji na saba wengine walihusishwa na wizi wa ngawira.

  Ripoti kamili ya Umoja wa Mataifa juu ya shutuma za ukiukwaji inatarajiwa kutolewa mwezi Januari mwakani.

  You May Like

  Jioni

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa waandishi wetu sehemu mbali mbali duniani na kote Afrika Mashariki na Kati, na vile vile vipindi na makala maalum kuhusu afya, wanawake, jamii na maendeleo.

  VOA Express

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za mchana na maelezo ya maswala yanayohusu vijana na wanawake. Matangazo haya yanafuatilia habari zilizojitokeza nyakati za mchana na ripoti za kina za habari ambazo hazisikiki sana katika matangazo mengineyo. VOA Express pia inafuatilia kwa karibu sana maswala yanayovuma katika mitandao ya kijamii kama sehemu moja muhimu ya upashanaji habari siku hizi.
  Alfajiri

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za michezo.

  mjadala huu umefungwa
  Comment Sorting
  Maoni
       
  Na: anania Kutoka: S A
  21.12.2012 02:06
  Shukurani kwa raisi Obama kwa kumuonya Kagame kuhusu uungaji wake mkono M23.Maskini wa Kongo wana uwawa bila hatiya yoyote Obama saidia Drc hasa S/kivu na N/kivu.