Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:21

Obama alaani polisi kufyatuliwa risasi huko Ferguson


Rais Obama akiwa katika kipindi cha "Jimmy Kimmel Live" ambapo alikemea tukio la polisi kupigwa risasi huko Ferguson
Rais Obama akiwa katika kipindi cha "Jimmy Kimmel Live" ambapo alikemea tukio la polisi kupigwa risasi huko Ferguson

Rais wa Marekani Barack Obama alikemea kupigwa risasi kwa maafisa wawili wa polisi kufuatia mashtaka ya ubaguzi wa rangi katika mji wa Ferguson, katika jimbo la Missouri, akiita ni hatua ya kihalifu na alisema mfyatuaji risasi au wafyatuaji risasi wanahitajika kukamatwa.

Bwana Obama alizungumza Alhamis usiku kwenye televisheni moja ya Marekani inayoendesha kipindi cha “Jimmy kimmel Live” alisema hakuna kisingizio kwa ufyatuaji risasi huo na hautakiwi kuhusishwa na suala linaloendelea huko.

Mwanasheria mkuu, Eric Holder
Mwanasheria mkuu, Eric Holder

Awali mwanasheria mkuu wa Marekani, Eric Holder aliliita shambulizi la Alhamis asubuhi ni la kushtukiza na alisema mhalifu alikuwa akijaribu kupanda mbegu ya mfarakano. Alimuita mfyatuaji risasi huyo ni mtu asiye na maana kabisa kwa watu.

Ufyatuaji risasi huo umefanyika saa kadhaa baada ya mkuu wa polisi katika mji wa Ferguson kujiuzulu kufuatia ripoti ya wizara ya sheria iliyoshutumu mwenendo wa idara hiyo ambao umeegemea katika ubaguzi wa rangi.

Alhamis polisi walimsaka mfyatuaji risasi lakini hawakufanya ukamataji wowote huku darzeni ya watu walikusanyika kwa ajili ya maombi karibu na eneo lililotokea ufyatuaji risasi na waandamanaji waliendelea kufanya maandamano yao wakipita kituo cha polisi.

Aliyekuwa mkuu wa polisi Ferguson, Thomas Jackson
Aliyekuwa mkuu wa polisi Ferguson, Thomas Jackson

Mkuu wa polisi wa mji wa Ferguson, Thomas Jackson aliwasilisha barua yake ya kujiuzulu Jumatano ikiwa ni miezi saba baada ya kuzuka mvutano juu ya ubaguzi wa rangi kufuatia ofisa polisi mzungu, Darren Wilson kumfyatulia risasi na kumuua kijana mweusi asiye na silaha, Michael Brown baada ya Brown kumshambulia polisi wakati wa mzozo wa mtaani uliotokea mwezi Agosti mwaka jana.

Jackson alikuwa kiini cha malalamiko yenye ghadhabu kuhusu ubaguzi wa rangi ndani ya idara yake ya polisi kufuatia ufyatuaji risasi wa brown. Ripoti ya wizara ya sheria iliikosoa idara ya polisi ya Ferguson kwa kutotenda haki dhidi ya wakazi weusi walio wengi katika mji huo, ikiwemo kusimamishwa barabarani bila sababu ya msingi, ukamataji holela na dereva kupatiwa tiketi za bila sababu ya msingi. Ripoti ilisema maafisa wa mji waliendesha mahakama zao kama kituo cha kupatia fedha.

Jackson ni ofisa wa sita katika mji wa Ferguson kujiuzulu kufuatia ripoti ya wizara ya sheria. Meneja wa mji wa Ferguson na jaji wa mahakama katika halmashauri ya mji huo walijiuzulu pia wiki hii huku mfanyakazi mmoja wa mahakama ya mji huo na maafisa wawili wa polisi walitakiwa kuacha kazi au kujiuzulu baada ya kuonekana kwenye ripoti hiyo wakituma barua pepe zinazohusu ubaguzi wa rangi.

Maandamano kufuatia kifo cha Michael Brown
Maandamano kufuatia kifo cha Michael Brown

Ferguson ni kiunga kilichopo ndani ya mji wa St. Louis bado unakumbuka tukio la ufyatuaji risasi, ambalo limechochea siku kadhaa za ghasia katika mji. Ofisa Wilson hakufunguliwa mashtaka na wizara ya sheria kwa kukiuka haki za kiraia za Brown na baraza la mahakama lilishindwa kumfungulia mashtaka dhidi yake.

XS
SM
MD
LG