Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 22:36

Obama aelekea majimbo ya wa-Conservative


Rais Obama akizungumza katika chuo kikuu cha Boise huko Idaho kufuatia hotuba yake ya jumanne
Rais Obama akizungumza katika chuo kikuu cha Boise huko Idaho kufuatia hotuba yake ya jumanne

Siku moja baada ya kutoa hotuba yake ya hali ya kitaifa kwa bunge jipya la Marekani linaloongozwa na Republican, Rais Barack Obama anaelekea kwenye maeneo ya wa-Conservative nchini Marekani kuhamasisha kipengele cha hotuba yake, mpango wa kuboresha daraja la kati.

Bwana Obama aliondoka Washington jumatano kwa ziara ya siku mbili kuelekea Idaho na Kansas. Alitarajiwa kuwaambia wasikilizaji kwamba kila mtu ataona mafanikio ya uchumi ambao kwa jumla umefufuka kutoka miaka kadhaa ya kudorora.

Maafisa wa White House walisema Rais alichagua makusudi majimbo ya wa-Conservative kuwa vituo vyake vya kwanza kuzungumzia hotuba yake ya kila mwaka kwa bunge. Katika hotuba yake jumanne jioni bwana Obama aliwaambia wabunge na mamilioni ya watu waliotazama hotuba hiyo kupitia televisheni kwamba ni wakati wa kufungua kurasa mwingine kutoka hali ya kudorora kwa uchumi na vita na kufanya kazi pamoja kuboresha wamarekani wa daraja la kati.

Rais Obama (L) akipeana mikono na watu mbalimbali baada ya hotuba ya jumanne
Rais Obama (L) akipeana mikono na watu mbalimbali baada ya hotuba ya jumanne

Alizungumzia sera kama kupandisha kodi kwa matajiri na kuwapa wanafunzi fursa ya kwenda vyuo vya kijamii bure kwa miaka miwili. Baada ya kuona chama chake cha Democrat kimepoteza udhibiti wa baraza la seneti na kuchukuliwa na wa-Republican katika uchaguzi wa katikati ya awamu mwezi Novemba mwaka jana bwana Obama amechukua jukumu zaidi la sera kutoka mageuzi ya uhamiaji kuelekea kuboresha uhusiano na Cuba huku akiwa anatengeneza hiba yake.

Ukusanyaji maoni unaonesha kiwango chake cha utendaji kimepanda. Mipango ya bwana Obama inazuiliwa na wa-Republican ambao hivi sasa wanadhibiti bunge.

XS
SM
MD
LG