Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 16:45

Ndege ya Malaysia imeanguka huko Ukraine


Mabaki ya ndege ya Malaysia Boeing 777 yameonekana karibu na Grabovo katika mji wa Donetsk, July 17, 2014.
Mabaki ya ndege ya Malaysia Boeing 777 yameonekana karibu na Grabovo katika mji wa Donetsk, July 17, 2014.

Ndege ya Malaysia iliyokuwa ikisafiri kutoka Amsterdam kuelekea Kuala Lumpur imeanguka huko mashariki mwa Ukraine katika mkoa wa Donetsk ambao unashuhudia mapigano makali kati ya majeshi ya serikali ya Ukraine na waungaji mkono wa Russia wanaotaka kujitenga.

Ofisa mmoja wa wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine Anton Gerashchenko alisema ndege hiyo ilitunguliwa na kombora.

Ndege hiyo aina ya Boeing 777 ilikuwa imebeba abiria 288 na wafanyakazi wa ndege 15.

Moshi na mabaki ya ndege ya Malaysia Boeing 777
Moshi na mabaki ya ndege ya Malaysia Boeing 777


Rais wa Ukraine Petro Poroshenko alisema ametuma salamu za rambi rambi kwa waziri mkuu wa Uholanzi akiongeza kuwa tukio hilo halikuwa ajali au dhoruba lakini ni kitendo cha ugaidi.

Wakati huo huo Rais Barack Obama alizungumza Alhamis kwa muda mfupi kuhusu ajali hiyo mwanzoni mwa mkutano uliopangwa wa waandishi wa habari katika jimbo la Delaware nchini Marekani. “Hivi sasa tunafanya kazi ya kuangalia iwapo kulikuwa na raia wa Marekani kwenye ndege hiyo. Hicho ndicho kipaumbele chetu cha kwanza”.

Pia aliahidi msaada wa Marekani katika kusaidia kujua nini kilichosababisha ndege hiyo kuanguka. “Marekani itatoa msaada wa aina yeyote tutakaoweza ili kuchunguza nini kilichotokea na kwa nini. Na kama nchi fikra na dua zetu zipo na familia pamoja na wasafiri popote pale wanapopaita nyumbani”.

XS
SM
MD
LG