Jumanne, Mei 26, 2015 Local time: 14:32

Habari / Afrika

Mtwara watofautiana na serikali kuhusu bomba la gesi

Mitambo ya kuchimba mafuta
Mitambo ya kuchimba mafuta
Mvutano mkubwa umezuka nchini Tanzania baina ya serikali na wananchi wanaotoka mkoa wa Mtwara ambao  wanapinga hatua ya serikali kuweka bomba litakolotumika kusafirisha gesi kutoka mkoani humo hadi mkoani Dar es Salaam.

George Njogopa, Tanzania
George Njogopa, Tanzaniai
|| 0:00:00
...    
🔇
X

Wakati serikali ikiendelea kusisitiza nia ya kuendelea na hatua hiyo  mamia ya wananchi wa mkoa wa Mtwara wakiungwa mkono na wabunge wao wanaitaka serikali kusitisha zoezi hilo na badala yale uendeshwaji wa gesi hiyo ufanyike ndani ya mkoa wa Mtwara  eneo ambalo limegunduliwa kuwa na gesi nyingi nchini humo.
 
Tayari Rais Jakaya Kikwete na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospita Mhongo wamezungumzia sakata hilo na kuwataka wananchi hao kuyaweka kando madai yao kwa maelezo kuwa rasilimali zinazoendelea kugundulika ndani ya nchi zitatumika kwa manufaa ya wananchi wote.
 
Mvutano kuhusu wapi iendelezwe gesi hiyo umezidi kuchukua sura mpya baada ya hivi sasa kujitokeza viongozi wa kidini na kutangaza kuwa wanaunga mkono madai yaliyotolewa na wananchi wa mkoa wa Mtwara ambao wanasisitiza kuwa wananyang’anywa  rasilimali zao.
 
Kufuatia hali hiyo  mwenyekiti wa chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia amezitolea wito pande zote kuwa na majadiliano ya pamoja na hatimaye kutoa suluhisho litakolosaidia uendelezwaji wa rasilimali hiyo.
 
Wakati huo huo makundi ya wanaharakati hivi karibuni yalikutana na kujadiliana kwa kina sera mpya iliyotolewa na serikali kuhusu  sekta ya gesi. Pamoja na mambo mengine makundi hayo ya wanaharakati yalikosoa na kuipinga sera hiyo wakidai  kuwa imejaa  mapungufu.
 
Wananchi wa eneo la Mtwara pia wameokosoa sera hiyo kwa madai kuwa hawakushirikishwa wakati wa kuandaliwa kwake.
 
Baadhi ya wabunge kutoka chama tawala cha CCM, wameunga mkono madai yanayotolewa na wananchi hao na wengine wakisisitiza kuwa wako tayari kuchukuliwa hatua zozote na chama  lakini wataendelea kutetea hoja za wananchi wao.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.