Jumatatu, Mei 25, 2015 Local time: 10:15

Habari / Afrika

Morsi afupisha ziara kufuatia ghasia za Cairo

Waandamanaji wanaompinga rais Morsi wakirusha mawe kwa polisi wa kutuliza ghasia mjini Cairo, January 25, 2013.
Waandamanaji wanaompinga rais Morsi wakirusha mawe kwa polisi wa kutuliza ghasia mjini Cairo, January 25, 2013.
Rais wa Misri Mohamed Morsi anafanya ziara fupi kuelekea Ujerumani, jumatano huku matatizo ya kisiasa nchini kwake yakiendelea kwa siku kadhaa za maandamano.
 
Bwana Mosri alifuta  ziara yake ya pili iliyopangwa mjini Paris na kurejea Cairo.
Watu wawili waliuwawa katika mji mkuu jumatano katika mapambano kati ya waandamanaji waliokuwa wakirusha mawe na polisi ambao walijibu kwa kutumia gesi ya kutoa machozi. Wataalamu wa huduma za afya walisema waathirika walipigwa risasi lakini haikufahamika wazi nani aliwafyatulia risasi hizo.

Waandamanaji wamekuwa wakiandamana nchini Misri tangu alhamisi siku  ambayo ilikuwa ni  maadhimisho ya miaka miwili ya ghasia  zilizomuondoa madarakani Rais wa zamani Hosni Mubarak. Zaidi ya watu 50 wamekufa tangu maandamano yalipoanza.

Kiongozi wa upinzani Mohamed ElBaradei alitoa wito wa jumatano kuwepo na mjadala wa  kitaifa wa kujaribu kusitisha ghasia hizo. Bwana Morsi alikubali jumapili kushiriki katika mazungumzo lakini chama kikuu cha upinzani cha National Salvation Front na makundi mengine yalikataa kushiriki kutokana na hali  ilivyo hivi sasa.

Rais alitangaza hali ya dharura ya kitaifa na kutoa amri ya kutotoka nje wakati wa usiku kuanzia jumatatu jioni ili kujaribu kusitisha maandamano yanayoipinga serikali katika miji ya Port Said, Ismailiya na Suez City.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.