Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 19, 2024 Local time: 05:55

Mmarekani-Msomali aenda Syria kujiunga na wenye msimamo mkali.


picha iliyotolewa na kundi la Islamic State (IS) ikimuinesha mfanyakazi wa misaada wa uingereza David Haines mwenye vazi la orenji akiwa amekamtwa na wanaosadikiwa kuwa wajumbe wa Islamic state.
picha iliyotolewa na kundi la Islamic State (IS) ikimuinesha mfanyakazi wa misaada wa uingereza David Haines mwenye vazi la orenji akiwa amekamtwa na wanaosadikiwa kuwa wajumbe wa Islamic state.

Mmarekani mwenye asili ya kisomali amesema mtoto wake wa kiume ametoroka marekani kwenda kujiunga na kundi la kiislamu lenye msimamo mkali nchini Syria.

Katika mahojiano maalumu na idhaa ya kisomali ya Sauti ya Amerika baba wa kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 Mohamud Mohamed amesema mtoto wake wa kiume aliondoka katika mji wa Minneapolis Julai 18 na akampigia mama yake simu akiwa Syria siku nne baadae na kumwambia alikuwa na ‘ kaka zake”.

Baba wa kijana huyo amesema Mohamed ambaye kwa kawaida anaishi na mama yake nchini Canada alikwenda Minneapolis kukaa naye kwa muda wakati wa kipindi cha mwezi mtukufu wa ramadhani. Amesema Mohamed alitoweka bila tahadhari akisema alikuwa anaenda msikitini kwa ajili ya sala za Ijumaa.

Amesema ilikuwa mshtuko. Mtoto wake alikuwa mwanafunzi alibadilika ghafla. Alikuwa anasali lakini aliongeza kusali masaa 24 na mara chache sana alikuwa mbali na misikiti. Alipanga safari yake bila baba yake kujua na akaishia Syria. Anasema wote katika familia wameshtushwa sana, hawakutegemea angeweza kufanya hivyo.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 19 alikwenda Uturuki njia ambayo inatumiwa na watu wa nchi za magharibi wanaotaka kujiunga na Islamic State na makundi mengine ya wanamgambo yanayofanya operesheni zake nchini Syria.

Hadithi yake ni sawa na ya wasomali wengine waliondoka marekani wakitaka kwenda kupigana sambamba na makundi kama hayo. Wasomali wawili kutoka jimbo la Minesota Abdiraham Muhumed na Douglas MacArthur McCain wameuwawa katika mapigano nchini Syria.

XS
SM
MD
LG