Jumamosi, Mei 30, 2015 Local time: 07:17

Habari / Afrika

Mlipuko mwingine wauwa watu 7 Nairobi

Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya wakiwa katika moja ya milipuko iliyotokea awali huko Kenya
Wafanyakazi wa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya wakiwa katika moja ya milipuko iliyotokea awali huko Kenya
Shirika la Msalaba Mwekundu nchini Kenya linasema  takriban watu saba waliuawa  na wengine 29 kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea kwenye basi ndogo la abiria mjini Nairobi Jumapili.
 
Mlipuko huo unafuatia mashambulizi kadha ya guruneti katika maeneo mbalimbali ya Kenya yanayotuhumiwa kutekelezwa na  wanamgambo wa Somalia wa al-Shabab. Haikubainika mara moja  kilichosababisha mlipuko kwenye basi la abiria maarufu kama  “Matatu”  linalobeba  hadi abiria 25 katika mtaa wa Eastleigh  mjini Nairobi. Lakini baadhi ya mashahidi na maafisa wa polisi walisema walimwona mtu akilitupia  guruneti gari  hilo.
 
Mwandishi wa Sauti ya Amerika-VOA aliyefika mahala pa tukio hilo alisema ilionekana kama mlipuko huo ulisababishwa na bomu la kutengenezwa nyumbani.  Mlipuko huo ulikuwa mkubwa kiasi cha kuliteketeza kabisa  basi hilo ndogo la abiria.
 
Shahidi mmoja Mohammed Qadar Gudle  alisema alisikia mlipuko huo akiwa umbali wa mita 500 kutoka eneo la tukio hilo. Gudle anasema mapigano yalizuka mara tu baada ya mlipuko  huo  kwenye mtaa wa Eastleigh na watu wenye hasira wakawageukia na kuwapiga wasomali katika mtaa huo.
 
Katika miezi ya karibuni Kenya imekabiliwa na mashambulizi ya guruneti katika makanisa na maeneo ya umma yakiwemo mashambulizi mawili ya guruneti katika mtaa huo wa Eastleigh wenye wakaazi wengi wa jamii ya Kisomali.

Polisi wa Kenya wanawalaumu wanamgambo wa al-Shabab kutoka  Somalia  kwa mashambulizi hayo  wakisema kundi hilo linalipiza kisasi  kwa mashambulizi ya jeshi la Kenya  dhidi ya al-Shabab nchini Somalia .
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Matatizo ya Miundombinu Dar Es Salaami
|| 0:00:00
...  
🔇
X
21.05.2015 05:17
Wakazi wa Dar es Salaam wanasema ukosefu wa miundo mbinu inayostahiki ndiyo inasababisha matatizo ya uchafu, huduma za maji na nishati.