Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 13:52

Mkutano wa APEC waanza Beijing

Rais wa China Xi Jingping akifungua rasmi mkutano wa APEC,Beijing, Nov. 9, 2014
Rais wa China Xi Jingping akifungua rasmi mkutano wa APEC,Beijing, Nov. 9, 2014

Uchumi wa China ulididimia katika robo tatu ya mwaka na kufikia viwango visivyoonekana tangu mwaka wa 2008 na 2009 wakati uchumi wa dunia ulipodhoofika sana.

Rais wa China Xi Jingpin, amefungua rasmi sherehe za kila mwaka za mkutano wa jumuiya ya ushirikiano wa kiuchumi wa Asia-Pacific –APEC , akisema hakuna haja ya kuwa na wasiwasi kutokana na uchumi wa China unaokua polepole.

Bw. Xi aliwaambia viongozi wa kibiashara duniani mjini Beijing Jumapili, kuwa China imejitolea kufanya mabadiliko ya kina ili kutoa fursa kwa masoko kuwa na ushawishi mkuwa kwa uchumi.

Uchumi wa China ulididimia katika robo tatu ya mwaka na kufikia viwango visivyoonekana tangu mwaka wa 2008 na 2009 wakati uchumi wa dunia ulipodhoofika sana.

Naye rais wa Marekani Barack Obama aliondoka Washington mapema Jumapili kwa ziara itakayompeleka China kwa mkutano huo wa APEC kabla ya kuelekea Myanmar- inayojulikana pia kama Burma na kisha Australia kwa mkutano wa G20

XS
SM
MD
LG