Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 11:18

Mji wa Timbuktu waokolewa na majeshi ya Ufaransa


Wanajeshi wa Mali wakiwa kwenye kituo cha ukaguzi kwenye barabara ya Gao. Jan. 27, 2013.
Wanajeshi wa Mali wakiwa kwenye kituo cha ukaguzi kwenye barabara ya Gao. Jan. 27, 2013.
Majeshi ya Mali yamechukua udhibiti kwenye uwanja wa ndege na barabara inayoingia kwenye mji wa Timbuktu nchini Mali huku wakiendelea na operesheni ya kuwaondoa wanamgambo wa ki-Islam ambao wamedhibiti upande wa kaskazini mwa Mali kwa miezi kadhaa.

Maafisa wa jeshi walisema jumatatu kuwa majeshi ya anga na ya ardhini yakisaidiwa na helikopta yalifanikiwa kuingia mjini humo wakati wa usiku.

Idara inayohusika na masuala ya utamaduni katika Umoja wa Mataifa UNESCO imeiorodhesha Timbuktu kama eneo la World Heritage kwa ajili ya kuwa na misikiti na majengo ya kiasili ambayo baadhi ya tangu karne ya 15. Lakini kundi la ki-Islam la Ansar Dine linaliona eneo hilo kuwa la kufuru na wanamgambo wameharibu baadhi ya makaburi ya asili mjini humo.

Meya wa Timbuktu alisema jumatatu kuwa wanamgambo wa ki-Islam wanaokimbia mjini humo wamechoma moto kwenye maktaba yenye maelfu ya nakala za kihistoria.

Mji wa Timbuktu upo kilomita 300 kaskazini-magharibi mwa Gao ambako majeshi ya Ufaransa na Mali yalichukua tena udhibiti jumamosi kutoka kwa wanamgambo wa ki-Islam ambao walikimbia bila ya kufanya upinzani.
XS
SM
MD
LG