Jumanne, Februari 09, 2016 Local time: 00:01

  Habari

  MERRY KRISMAS

  Baba Mtakatifu Benedict akisalia misa ya mkesha wa Kristmas katika kanisa la St. Peter's Basilica Vatican Dec. 24, 2012
  Baba Mtakatifu Benedict akisalia misa ya mkesha wa Kristmas katika kanisa la St. Peter's Basilica Vatican Dec. 24, 2012
  Baba Mtakatifu Benedict ameombea amani, hasa Mashariki ya Kati, katika misa yake ya mkesha wa Krismas, wakati wakristo kote duniani wanajiandaa kusherehekea leo kuzaliwa kwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2,000 iliyopita.

  Akihutubia waumini katika kanisa la Mtakatifu Petro Jumatatu jioni, kiongozi huyo wa kanisa katoliki alitoa wito wa kumaliza umwagaji damu Syria, Lebanon, Iraq na nchi za jirani. Aliombea pia watu wa Israel na Palestina kuishi pamoja kwa amani.

  Maelfu wa watalii kutoka kote duniani walikusanyika katika mji wa Bethlehem, Ng'ambo ya Magharibi kusherehekea sikukuu hiyo mahali ambapo Wakristo wanaamini Yesu Kristo alizaliwa.

  Jumanne maelfu ya Wakristo kote duniani watamiminika katika makanisa kuhudhuria misa ya krismas na kufuatiwa na sherehe ikiwa ni chakula, vinywaji na kutembeleana. Katika nchi za Afrika Mashariki na Kati wakristo wengi wanatazamiwa kusherehekea kwa mikusanyiko ya kila namna kuanzia starehe hadi ibada.

  Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika inawatakiwa wasikilizaji wetu wote Krismas Njema

  You May Like

  sauti Wachambuzi waonya kuhusu mzozo wa Zanzibar

  Wadadisi wanasema kwamba mvutano huo utamalizwa na Wazanzibari wenyewe. Zaidi

  sauti Wafuasi wa MRC wadai kuandamwa na serikali

  Wafuasi hao sasa wanaitaka mahakama ya juu Kenya kuweka wazi suala la uhalali wa vuguvugu la MRC ambalo wakati mmoja liliishitaki serikali kwa kuwajumuisha kuwa miongoni mwa makundi haramu. Zaidi

  Facebook yaanzisha huduma ya video za moja kwa moja

  Mtandao wa kijamii wa Facebook umeongeza huduma nyingine  ambayo imepokelewa kwa furaha na baadhi ya wateja. Facebook inwawezesha baadhi ya wateja wake kuwasiliana kupitia video ya moja kwa moja, huduma ambayo haikuwepo hapo awali isipokuwa kwa wale waliotumia simu aina ya Iphone hapa Marekani. Zaidi

  Sanders na Trump waongoza kura ya maoni

  Kwa upande wa wademokrat Sanders anaongoza kwa alama 10 dhidi ya waziri wa mambo ya nje wa zamani Hillary Clinton Zaidi

  katika picha Kampeni za Uchaguzi wa Awali za pamba moto Marekani

  wagopmbea kiti cha rais hapa Marekani wako katika awamu ya pili muhimu ya uchaguzi wa awali ambapo kuna baadhi watalazimika kuamua kuendelea au kuondoka. Zaidi