Jumamosi, Mei 25, 2013 Local time: 02:20

Habari / Afrika

Mazungumzo ya DRC kuanza Ijumaa Kampala

Wapiganaji wa M23 wakiondoka karibu na mji wa Sake kiasi cha kilomita 42 magharibi mwa Goma Novemba 30,2012
Wapiganaji wa M23 wakiondoka karibu na mji wa Sake kiasi cha kilomita 42 magharibi mwa Goma Novemba 30,2012
ukubwa wa habari - +
Waasi huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Ijumaa watafanya mazungumzo na serikali ya Congo.

Msemaji wa serikali ya Uganda Fred Opolot anasema wajumbe kutoka serikali ya Congo na kundi la waasi la M23 wataanza vikao vya awali mjini Kampala vitakavyolenga namna ya kutatua mgogoro wao.
 
Anasema mazungumzo yatalenga juu ya kanuni za msingi kwa  mikutano ya baadae na miongozo kwa  waangalizi ambao watafuatilia  maeneo ya mzozo huko mashariki mwa DRC.

Kundi la m23 liliondoka kutoka mji wa Goma uliopo mashariki mwa DRC wiki iliyopita lakini kundi hilo linatishia kuuteka tena mji huo  kama serikali inashindwa kuanza mashauriano.
Waasi walilishinda  jeshi la Congo katika mifululizo kadhaa ya mapigano mwaka huu.

Jopo moja la wataalamu wa Umoja wa Mataifa linaishutumu Uganda na Rwanda kwa kulisaidia kundi la waasi kitu ambacho nchi zote zinakanusha.
 
Taarifa ya Alhamis kutoka kwa Opolot ilisema “Uganda kama mwenyekiti wa sasa wa mkutano wa kimataifa wa eneo la maziwa makuu inaendelea kuratibu utaratibu wa amani huko DRC”.
 
Kundi la M23 limeundwa na waasi wa zamani ambao waliingizwa  katika jeshi la Congo kufuatia  mkataba wa amani wa mwaka 2009. Waasi walijitoa kwenye jeshi mapema mwaka huu wakidai kubaguliwa na kupatiwa  huduma mbaya.

Mapigano yamewakosesha makazi zaidi ya watu 100,000 katika jimbo la Kivu kaskazini huko Congo na kusababisha kuwepo hali mbaya ya kibinadamu katika eneo hilo.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one

Mitaani

Loading
12:00:00 / -:--:--