Jumatatu, Machi 30, 2015 Local time: 04:02

Habari / Afrika

Mazungumzo ya amani ya DRC yapiga hatua

Kiongozi wa kundi la waasi wa M23 Askofu Jean Marie Runiga, akizungumza na waandishi habari, Bunagana, Congo, Jan. 3, 2013.
Kiongozi wa kundi la waasi wa M23 Askofu Jean Marie Runiga, akizungumza na waandishi habari, Bunagana, Congo, Jan. 3, 2013.
Mazungumzo ya amani mjini Kampala kati ya serikali ya Jamhuri ya demokrasi ya Congo na waasi wa M23 yamepiga hatua kubwa baada ya pande zote mbili kukubaliana kuhusu kipengele cha kwanza cha ajenda ya mkutano huo ambacho kilikuwa cha kuutekeleza mkataba uliotiwa saini mwaka wa 2009 kati wa serikali ya Congo na waasi wa CNDP.

Na kama anavyoripoti mwandishi wetu wa Kampala Leylah Ndinda, pande zinazozozana zilikubaliana kuwa mazungumzo yao yatakuwa na maswala manne muhimu yatakayojadiliwa.Kwanza kuutekeleza  mkataba kati ya serikali ya Congo na waliokuwa waasi wakati huo wakijiita CNDP ambao baadhi yao waliasi jeshi na kuunda jeshi la M23, pili, usalama nchini Congo, tatu kuzitatua shida za kisiasa, uchumi na jamii na mwisho njia ya kutekeleza makubaliano yatakayofikiwa mjini Kampala.

Kwenye kikao cha kumi na tatu, baada ya kupitia vipengele vyote vya mkataba wa 2009, pande zote mbili zilisema mkataba huo ulikuwa mzuri na kisha kugawa vipengele vya mkataba huo  mara tatu. Vile vilivyotekelezwa kamili, vile ambavyo havikutekelezwa kikamilifu  na vile ambavyo havikutekelezwa kamwe.

Vipengele 15 vilitekelezwa kikamilifu, 8 vikatekelezwa kiasi, na kumi na mbili havikushughulikiwa hata kidogo.Kutekelezwa kwa mkataba huu kulifaa kufanywa na pande zote mbili lakini kila upande haukutekeleza majukumu yake kikamilifu.

Kwa mfano, serikali ilitakiwa kuunda kikosi cha polisi wa vijijini kuwalinda raia lakini haikufanya hivyo. Waasi nao walitakiwa kuhakikisha kuwa ikiwa wana shida zozote wanazitatua kulingana na sheria na sio kwa kuchukua silaha lakini walirejelea silaha mwaka uliopita.
 
Baadhi ya mafanikio ya mkataba huo yalikuwa serikali kuwasamehe waasi wa CNDP na waasi kujiunga na jeshi la serikali ya DRC.
mjadala huu umefungwa
Comment Sorting
Maoni
     
Na: KARUBANDIKA KIBALO Kutoka: Lexington, KY
08.02.2013 06:05
Tuna tambuwa kama hawa watu wa Serikali ya Kinshasa pamoja na Waasi wa M23 Wanaendelea kufanya njama ya Kuendelea na kuangamiza Raia ya CONGO juu ya Tumbo zao, Kwa nini yeye Kabila hawezi tosheka na yenye aliisha Iba katika inchi ya CONGO yeye na watu wake? anataka awe kama Bwana Mobutu, atolewe kwa haya na ashindwe kurudi mu inchi kwenye alitawala? anapenda afiye uhamishoni kama Madictator wote? Muwe na Huruma ya Binadamu , Viumbe vya Mungu , Mungu Hapendi mtu wa kutesa Kiumbe alichoumba....Muwe hange nawaonya kwa mara ya Mwisho, kama munashupaza shingo mutakufa vibaya.

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • Je Nifanyeje?
  30 min

  Je Nifanyeje?

  Je Nifanyeje? Maamuzi ya Afya na Kijamii kwa Vijana - Kipindi cha dakika 30...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Waandamana kupinga ubakaji Kenyai
|| 0:00:00
...  
🔇
X
27.03.2015 18:06
Mamia ya wanawake nchini Kenya hivi majuzi walishiriki maandamano kupinga vitendo vya ubakaji ambayo vimekithiri nchini humo