Ijumaa, Machi 27, 2015 Local time: 16:09

Habari / Afrika

Marekani na AU wataka M23 wadhibitiwe

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton(R) na mwenyekiti wa AU, Nkosazana Dlamini-Zuma(L)
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton(R) na mwenyekiti wa AU, Nkosazana Dlamini-Zuma(L)
Marekani na Umoja wa Afrika zinahimiza hatua ichukuliwe mara moja  ya kupelekea kikosi kisichoegemea upande wowote katika maeneo ya mashariki mwa Congo yanayokaliwa na waasi kwenye mpaka  wa nchi hiyo na Rwanda.

Waziri wa  mambo ya nje  wa Marekani, Hillary Clinton amesema ni sharti Rwanda  isaidie  kuzuia uungaji mkono wa uasi huo.  Kundi la waasi hao wa M23 limesema linajiandaa kuondoa udhibiti wake kwenye mji wa Goma, lakini maafisa wa Marekani wamesema ni mapema mno kubaini ikiwa kundi hilo linaondoka au lina mpango mwingine wa kijeshi.
 
Katika mkutano uliofanyika kwenye wizara ya mambo ya nje ya Marekani akiwa na mwenyekiti wa  Umoja wa  Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, Waziri Clinton amesema njia pekee kwa waasi hao ni kutii mkataba uliofikiwa nchini Uganda.  Kama sehemu ya mkataba huo, Rais wa Congo Joseph Kabila, Yoweri Museveni wa Uganda na Paul Kagame wa Rwanda walikubaliana juu ya kupelekwa kikosi kisichoegemea upande wowote kuchukua udhibiti wa maeneo yanayokaliwa na waasi.

Lakini mkataba huo umegubikwa na utata kwa sababu kuna dhana kuwa Rwanda ndiye muungaji mkono mkuu wa waasi hao wa M23, dai ambalo Rwanda inakanusha.  Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Dlamini Zuma anasema  kuungana pamoja kwa viongozi wa ukanda huo kuzima mapigano ni muhimu zaidi kuliko kulaumiana. Waziri Clinton pia alisisitiza kuwa sharti viongozi wote wachukue  hatua kuzuia kundi hilo la waasi kupata uungaji mkono wa aina yoyote ile.
 
Mapigano mashariki mwa Congo yamepelekea watu 285,000 kukimbia nyumba zao katika muda wa miezi minane iliyopita  na kusababisha kile waziri Clinton anasema ni madhara makubwa ya kibinadamu huku wafanyakazi wa afya  huko Goma wakiuawa na hata wengine kutekwa nyara.
mjadala huu umefungwa
Maoni
     
There are no comments in this forum. Be first and add one
 • Alfajiri
  30 min

  Alfajiri

  Matangazo ya nusu saa kuhusu habari za mapema asubuhi pamoja na habari za...

 • Jioni
  30 min

  Jioni

  Matangazo ya saa nzima kuhusu habari za kutwa, ikiwa ni pamoja ripoti kutoka kwa...

 • VOA Express
  30 min

  VOA Express

  VOA Express ni matangazo mapya yenye mwendo wa kasi yakiangalia habari mpya za...

Mitaani

Your JavaScript is turned off or you have an old version of Adobe's Flash Player. Get the latest Flash player.
Ajali barabarani Tanzania zaongezekai
|| 0:00:00
...  
🔇
X
18.03.2015 16:17
Matukio ya ajali mbaya za barabarani Tanzania hivi karibuni zinasemekana kuwa ishara ya ongezeko la uzembe na kutozingatia sheria za usalama barabarani, kulingana na watalaam.